FT: Algeria 0-0 Tanzania | AFCON Qualifier | Tanzania yafuzu AFCON

FT: Algeria 0-0 Tanzania | AFCON Qualifier | Tanzania yafuzu AFCON

Tuna kila sababu ya kufurahi leo bila kujali nini kitatokea mbele ya safari, watu wengi walielekea kuamini kuwa T stars haitavuka mbele ya Algeria. Uganda pia walidhani shughuli imeeisha licha ya kutuombea njaa sisi ndo tumefuzu.
 
Ivory Coast sio poa ndio maana tumenyeea mapema.
 
Mbinu za medani za muda wa nyongeza....

Bacca anasukumwa kidogo na kujirusha [emoji1787]

Wachezaji wetu wanahamaki(zuga) na kureact dhidi ya kusukumwa BACCA [emoji1787][emoji1787]

Kocha wetu anarusha chupa za maji ndani....[emoji1787]

All and all nitashuhudia fainali za pili za AFCON ndani ya maisha yangu alhamdulillah [emoji120]
Na sisi tumejanjaruka mkuu
 
Na huu ndiyo ukweli mchungu! Kama tumeshindwa kuwa na professional players wengi nje wa kuja kulisaidia Taifa kwenye mechi kama hizi, basi bora tukapunguza tu idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye ligi yetu.
Karia hataki kufeli kote, kaona hata akipunguza wageni kwenye ligi yetu bado wazawa hawawezi lisaidia taifa, ona mtu kama mzize leo alikuwa anafanya nini uwanjani? Karia karuhusu wageni wengi matokeo yanga anacheza fainali caf simba anashiriki super league
 
Taifa stars imetutoa kimasomaso Watanzania kwa kufuzu AFCON 2023 baada ya kutoka suluhu kule Algeria. Chakushangaza ni kuwa hakuna shamrashara kama vile wengi hawajafurahi. Ni kwann jaman?? Ebu tuchangamke basi na tuandae mapokezi ya kusisimua kwa heroes wetu
Shida watu wamebeti mihela mingi na kumpa Algeria ushindi,mikeka imechanika
 
Sana mkuu sema wachezaji waliofanikisha hili wawaache hadi mwisho isitokee tena kikosi kikabadilishwa watawakatisha tamaa.
 
Tunaipongeza sirikali ya awamu ya 6 chini ya Jemedari mbeba maono Mama Doctor Samia Suluhu kwa kutuheshimisha watanzania kwenye uga wa soka la kimataifa natambua juhudi za sirikali yako tukufu kuinua michezo mingine kama ngumi soka la kinamama na michezo mingine
makofi tazavalii
 
Taifa stars imetutoa kimasomaso Watanzania kwa kufuzu AFCON 2023 baada ya kutoka suluhu kule Algeria. Chakushangaza ni kuwa hakuna shamrashara kama vile wengi hawajafurahi. Ni kwann jaman?? Ebu tuchangamke basi na tuandae mapokezi ya kusisimua kwa heroes wetu
Labda ww na mke wako au mme wako
 
Back
Top Bottom