FT: AS Real Bamako 1-1 Young Africans | CAF Confederation Cup | Stade Modibo Keita | 26.02.2023

FT: AS Real Bamako 1-1 Young Africans | CAF Confederation Cup | Stade Modibo Keita | 26.02.2023

Kila la kheri chama langu
FB_IMG_16762896298059766.jpg
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizonifikia muda huu kutoka Mali ni kwamba yule striker kiboko wa Bamako ndio anaamka muda huu.

Unaweza kujiuliza kwanini kuamka kwake kuwe ni big agenda?

Ishu ni kwamba hajaamka kutokea kitandani, ameamka kutokea kwenye swimming pool naskia alilala chini ya maji akitafuta pumzi
 
Ni jumapili tulivu, wapenda kandanda tunakutana tena hapa jukwaani kushuhudia mechi za Kombe la Shirikisho Africa.

Leo katika kundi D, AS Real Bamako ya Mali inawakaribisha wawakilishi wa Tanzania Young Africans SC katika dimba la Stade Modibo Keita wenye uwezo wa kuchuku watazamaji 35,000. Uwanja hui umepewa jina la aliyepata kuwa Rais wa kwanza wa Mali.

Ikumbukwe AS Real Bamako, bado inatafuta ushindi wake wa kwanza, mara baada ya kufungwa mchezo wa kwanza na kudroo mchezo wa pili huku ikiwa na alama 1.

Kwa upande wa Young Africans, watashuka dimbani wakiwa na alama 3 baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kisha kushinda mchezo wa pili dhidi ya TP Mazembe wiki moja iliyopita.

Kama mjuavyo kwa mpira wa Afrika, timu iliyopo nyumbani ina nafasi kubwa ya kupata ushindi, je AS Real Bamako wataweza kupata ushindi wao kwanza? Au Yanga wataendeleza ushindi?

Mechi itapigwa Saa 1:00 Usiku kwa Masaa ya Afrika ya Mashariki, na kuwa mubashara kupitia, ZBC2 ya AzamTv na Variety 3 chaneli 228 ya DStv.

Live updates, utani wa hapa na pale, tambo na majigambo yote basi tukutane kwenye uzi huu...
Kila la heri timu la kwanza kuanzishwa Nchini Tanzania na lenye makombe mengi ya kutosha.
 
Ikiwa Man U atatwaa ubingwa basi itakuwa furaha kuu kwangu ikiwa ubingwa huo utaendana na kipigo kwa Vyura Fc .

Bamako fanya jambo jumapili yangu iwe sawa .

Saa sita nitaenda kunywa pombe ili niwezw kuisikia sauti ya nafsi yangu juu ya hii mechi stay tuned nitakuja na matokeo ya leo .
 
Ikiwa Man U atatwaa ubingwa basi itakuwa furaha kuu kwangu ikiwa ubingwa huo utaendana na kipigo kwa Vyura Fc .

Bamako fanya jambo jumapili yangu iwe sawa .

Saa sita nitaenda kunywa pombe ili niwezw kuisikia sauti ya nafsi yangu juu ya hii mechi stay tuned nitakuja na matokeo ya leo .
Hapo ndipo unapokosea ,wote washinde ndo itakuwa poa
 
Gongowazi [emoji196] ikifikia hatua hii mambo yanakuwa mazito kwao, wanakuwa hawana uwezo kwenye michuano ya Kimataifa, leo anapigwa na Real Bamako
 
Back
Top Bottom