FT: AS Real Bamako 1-1 Young Africans | CAF Confederation Cup | Stade Modibo Keita | 26.02.2023

FT: AS Real Bamako 1-1 Young Africans | CAF Confederation Cup | Stade Modibo Keita | 26.02.2023

Wanangu wa real Bamako hao wanyonyeni vinyeo hao kenge mana wanaupenda sana huo mchezo.

FT: BAMAKO 2 VS 0 VINYEO FC

MUNGU IBARIKI AFRIKA NA KILA LA KHERI REAL BAMAKO.
We kinyume nyume fc, acha wenge, wanaume wafanye yao.
Hao shoga zako watagongwa na kitu kizito watulie.
 
Timu yoyote yenye jina linaloanzia na Real haiwezi kuwa utopolo. Lazima heshma ya baba zao ilindwe.
 
Hapo ndipo unapokosea ,wote washinde ndo itakuwa poa
Washinde waende wapi ?
Mimi nahitaji wote tubaki ligi kuu yetu habari za mechi za kimataifa ni za waarabu tu .

Simuoni Simba chama langu akivuka hapa maana Horoya mh [emoji848]
 
Ni jumapili tulivu, wapenda kandanda tunakutana tena hapa jukwaani kushuhudia mechi za Kombe la Shirikisho Africa.

Leo katika kundi D, AS Real Bamako ya Mali inawakaribisha wawakilishi wa Tanzania Young Africans SC katika dimba la Stade Modibo Keita wenye uwezo wa kuchuku watazamaji 35,000. Uwanja hui umepewa jina la aliyepata kuwa Rais wa kwanza wa Mali.

Ikumbukwe AS Real Bamako, bado inatafuta ushindi wake wa kwanza, mara baada ya kufungwa mchezo wa kwanza na kudroo mchezo wa pili huku ikiwa na alama 1.

Kwa upande wa Young Africans, watashuka dimbani wakiwa na alama 3 baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kisha kushinda mchezo wa pili dhidi ya TP Mazembe wiki moja iliyopita.

Kama mjuavyo kwa mpira wa Afrika, timu iliyopo nyumbani ina nafasi kubwa ya kupata ushindi, je AS Real Bamako wataweza kupata ushindi wao kwanza? Au Yanga wataendeleza ushindi?

Mechi itapigwa Saa 1:00 Usiku kwa Masaa ya Afrika ya Mashariki, na kuwa mubashara kupitia, ZBC2 ya AzamTv na Variety 3 chaneli 228 ya DStv.

Live updates, utani wa hapa na pale, tambo na majigambo yote basi tukutane kwenye uzi huu...
safi japo umeme hakuna tunaomba muda huo uwepo
 
Back
Top Bottom