FT: ASEC Mimosas 3-0 Simba SC | CAF Confederation Cup | Stade de L' amitie General

mkuu acha utani,berkane afe kwake?![emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
hajui soka la kiafrica huyu anaendeshwa na mihemko .soka la Africa sio kama la ulaya ambalo timu iwe home iwe away winning chance bado itategemea na mwenye uwezo. lakini Africa ni tofauti ,yani Africa ni kama vile ukiwa home tayari una goli moja mkononi.
 
Sio mtaalamu wa soka lakini nikionacho mara zote Simba wanakawia sana kustukiza mashambulizi.

Wanafika golini kwa adui kisha wanasubiri adui ajipange ndio waanze sambusa zao goli kupatikana ni 1/10.

Wanafika golini au jirani na goli hata mita 20 hawa shoot. Wanataka kuingia na mpira langoni.

Ona magoli yaliyofungwa na Asec yote ni mita za kutosha na hakuna wa kuremba. Swali Simba wajiulize hawawezi ku geuka na ku shoot?

Naona watu pale mbele kuanguka anguka tu. Kibu akipokea pasi mara zote ataanguka tu. Boko vivyo hivyo. Kocha haoni hayo?

Ningetamani kuona Mkude na Bwalya wana shoot kila mmoja angalao mara 5 hata wakikosa wanajaribu. Wafanyie mazoezi jambo hilo.

Ningetamani kuona beki Mohamed ajifunze kwa Enock namna ya kuzuia washambuliaji matata anaweza sana.

Usajili ujao Simba isajili wabunifu pale mbele. Kongole kwa Morrison anaonesha umahiri na akili kubwa ya mpira.

Nimeumia lakini Simba bado ni timu nzuri irekenishe mapungufu.
 
kaburu arudi kwenye kamati ya usajili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…