FT: ASEC Mimosas 3-0 Simba SC | CAF Confederation Cup | Stade de L' amitie General

FT: ASEC Mimosas 3-0 Simba SC | CAF Confederation Cup | Stade de L' amitie General

Gendamarie anatakiwa afe 3
Bwahahaha

images (2).jpeg
 
mkuu acha utani,berkane afe kwake?![emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
hajui soka la kiafrica huyu anaendeshwa na mihemko .soka la Africa sio kama la ulaya ambalo timu iwe home iwe away winning chance bado itategemea na mwenye uwezo. lakini Africa ni tofauti ,yani Africa ni kama vile ukiwa home tayari una goli moja mkononi.
 
Sio mtaalamu wa soka lakini nikionacho mara zote Simba wanakawia sana kustukiza mashambulizi.

Wanafika golini kwa adui kisha wanasubiri adui ajipange ndio waanze sambusa zao goli kupatikana ni 1/10.

Wanafika golini au jirani na goli hata mita 20 hawa shoot. Wanataka kuingia na mpira langoni.

Ona magoli yaliyofungwa na Asec yote ni mita za kutosha na hakuna wa kuremba. Swali Simba wajiulize hawawezi ku geuka na ku shoot?

Naona watu pale mbele kuanguka anguka tu. Kibu akipokea pasi mara zote ataanguka tu. Boko vivyo hivyo. Kocha haoni hayo?

Ningetamani kuona Mkude na Bwalya wana shoot kila mmoja angalao mara 5 hata wakikosa wanajaribu. Wafanyie mazoezi jambo hilo.

Ningetamani kuona beki Mohamed ajifunze kwa Enock namna ya kuzuia washambuliaji matata anaweza sana.

Usajili ujao Simba isajili wabunifu pale mbele. Kongole kwa Morrison anaonesha umahiri na akili kubwa ya mpira.

Nimeumia lakini Simba bado ni timu nzuri irekenishe mapungufu.
 
Uongozi unacheza na mashabiki wakiona wanalalamika sana basi wachezaji watapewa motisha watacheza vzr mechi kadhaa watashinda mashabiki watatulia na mashabiki tumetifautiana kuna wale wenye mahaba yan hawataki baya waambiwe kwenye timu hata kama kuna shida kwa mimi SSC hata kama kipindi kile inashinda sikuwa na ile amani 100% kwa sababu hawajatibu tatizo SSC inahitaji maboresho makubwa sana kuna wachezaji wengi wanatakiwa wasepe pale hata kama wakicheza vzr mechi mbili tatu wanatakiwa watoke waje wapya wenye uwezo tuachane na haya mambo ya viongozi kucheza na akili za mashabiki kama kweli wanataka mafanikio kikosi lazima kifumuliwe
kaburu arudi kwenye kamati ya usajili
 
Back
Top Bottom