FT: Azam FC 0-0 Simba SC | Aprili 5, 2026 | Safari ya kuikimbiza Yanga ni ngumu

FT: Azam FC 0-0 Simba SC | Aprili 5, 2026 | Safari ya kuikimbiza Yanga ni ngumu

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Mbio za kuendelea kuifukuzia Yanga katika nafasi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara zimeendelea kuwa ngumu kwa Azam FC na Simba baada ya timu hizo kugawana pointi moja kila upande kutokana na matokeo ya 0-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Matokeo hayo ya yanaifanya Simba kuendelea kubaki nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 35 katika michezo 16, wakati Azam FC ikibaki nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 33 kwenye michezo 17. Yanga inaendelea kuongoza Ligi ikiwa na alama 41 katika michezo 17.

Full Time: NBC Premier League | Azam FC 0-0 Simba SC | Azam Complex | Aprili 5, 2026
IMG_5374.JPG

IMG_5377.JPG
NBC Premier League Jumapili hii ni Mzizima Derby, Azam FC na Simba SC kila mmoja kashinda mchezo wake uliopita.

Je, Jumapili hii nani kuendeleza wimbi la ushindi?

Mechi hii itapigwa Azam Complex kuanzia saa 1:00 usiku.

Wale wazee wa kuomba ban siku hizi hamna imani na timu zenu? Mmeishiwa pawa kabisaaaa!

Screenshot_20260405_004037_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom