FT: Azam FC 2-3 Yanga | Ligi Kuu | Uwanja wa Mkapa / 25.12.2022

FT: Azam FC 2-3 Yanga | Ligi Kuu | Uwanja wa Mkapa / 25.12.2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mchezo huu ni wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ikiwa kileleni katika nafasi ya kwanza wakati Azam FC ikiwa nafasi ya tatu.

AZAM vs YANGA: Katika mechi 11 walizokutana kwenye Ligi Kuu tangu msimu wa 2017/18, Yanga wameshinda mara nyingi zaidi huku sare zikiwa ni mbili pekee. Mchezo wa leo unatarajiwa kuanza saa 2:15 Usiku, usubiri dakika 90.

Azam Yanga.jpg
Presha kubwa ipo kwa pande zote mbili, kwani mbali na matokeo ya uwanjani, suala la usajili wa Feisal Salum kudaiwa kuondoka Yanga huku ikitajwa kuwa anaelekea Azam FC nalo linaongeza 'presha' baina ya pande hizo mbili, hasa kwa kuwa uhamisho haujakamilika na umeandamwa na kelele nyingi.

Azam.jpg

Kikosi cha Azam FC

Yanga.jpg

Kikosi cha Yanga
Mchezo unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa

Mchezo umeanza
2' Mayee anachezewa faulo, mchezo unasimama anatibiwa
4' Mchezo unaendelea, mayele anarejea uwanjani
5' Kasi ya mchezo bado haijachanganya
5' Shambulizi kwa Yanga, kichwa cha Dube kinatoka nje la lango
10' Adhabu kwa Yanga baada ya Dube kuchezewa faulo na Job, inapigwa inakuwa kona
14' Shuti la Sopu linalenga lango lakini kipa wa Yanga, Diarra anafanya kazi nzuri
16' Azam wanafanya mashambulizi mfululizo
19' Timu zote zinashambuliana kwa zamu
22' Moloko anakosa nafasi ya wazi, mpira unampita kwa kasi
25' Yanga wanamiliki mpira na kutengeneza mashambulizi
27' Gooooooooooooo Azam wanapata goli
Sopu anamalizia krosi nzuri ya Dube
30' Gooooooooooooooooooooo
Mayele anaisawazishia Yanga likiwa ni bao lake la 14 msimu huu katika Ligi Kuu
32' Gooooooooooooooo
Azizi Ki anafunga kwa shuti kali la nje ya 18
35' Azizi Ki anachezewa faulo, anatolewa nje kutibiwa
42' Azam wanaanza kujipanga mdogomdogo baada ya kufungwa magoli mawili ya haraka
45' Mayele anakaa chini kuashiria ameumia, wakati huo zinaongezwa dakika 2 za nyongeza

MAPUMZIKO
Kipindi cha pili kimeanza
46 Gooooooooooo
Yuleyule Abdul Suleiman 'Sopu' anaisawazishia Azam FC goli la pili
52' Sure Boy wa Yanga anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
55' Adhabu karibu na lango la Yanga, shuti linapigwa mpira unapaa juu
59' Yanick Bangala anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
67' Dube anapata nafasi karibu na lango, anapaisha juu ya lango
Mchezo umesimama kwa muda, Sopu kaumia wakati akiruka
68' Mchezo unaendelea
69' Mayele anapiga shuti linapaa juu ya lango la Azam FC
74' Sospeter Bajana wa Azam anapata kasi ya njano kwa kucheza vibaya
77' Farid Musa anafunga goli la tatu kwa Yanga, ni baada ya kipa wa Yanga kutema shuti la Azizi Ki
80' Yanga imeuchukua mchezo
86' Diarra yupo chini anatibiwa, aliposimama akapewa njano kwa kupoteza muda
90' Zinaongezwa dakika 4
90+4' Full Time, Yanga inashinda magoli 3-2
 
Mchezo huu ni wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ikiwa kileleni katika nafasi ya kwanza wakati Azam FC ikiwa nafasi ya tatu.

Presha kubwa ipo kwa pande zote mbili, kwani mbali na matokeo ya uwanjani, suala la usajili wa Feisal Salum kudaiwa kuondoka Yanga huku ikitajwa kuwa anaelekea Azam FC nalo linaongeza 'presha' baina ya pande hizo mbili, hasa kwa kuwa uhamisho haujakamilika na umeandamwa na kelele nyingi.

View attachment 2458026
Kikosi cha Azam FC

View attachment 2458030
Kikosi cha Yanga​
Kwa hiki kikosi, kweli nimeamini kuna mgogoro kati ya Yanga na Feisal! Hata benchi hayupo?
 
Back
Top Bottom