Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni PETER BANDA sio ABDI hebu tutolee mkosiPatashika ya Michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup kuendelea kupigwa leo Mei 14, 2022 ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, anakipiga na TP Lindanda Wana Kawekamo Pamba FC, katika hatua ya robo fainali kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mchezo unatarajiwa kuwa mkali hasa baada ya Pamba FC kutaka kuwavuruga Simba SC katika mipango yao ya kutetea ubingwa huu wa Kombe la Azam Sports Federation Cup.
Kocha wa Simba SC Pablo Franco Martin amesema kuwa anahitaji ushindi hivyo atapanga kikosi kamili kulingana na umuhimu wa mchezo huu.
"Michuano hii hakuna timu rahisi, huu ni mchezo muhimu kwetu tunahitaji kushinda ili kusonga mbele tutapanga kikosi kamili kwa wachezaji wote walio tayari kwa mchezo" amesema Kocha Pablo
Naye Kocha wa Pamba FC Athuman Kairo amesema kuwa wamakuja kupambana kupata matokeo ya ushindi.
"Tumekuja kupambana na Simba SC, tuajua kuwa ni timu kubwa, ngumu, nzuri, lakini sisi kama Pamba FC tunawaheshimu na tutacheza kwa nidhamu ili mwisho wa siku tupate ushindi na kuweza kusonga mbele kwenye nusu fainali" amesema Kocha Kairo.
Yote kwa yote ni dakika 90 za jasho na damu kuamua..Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku.. Usikose Ukaambiwa.
Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana
..... Ghazwat.....
======================
Wakati wowote mpira utaanza Uwanja wa Mkapa | Simba SC Vs Pamba FC
00' Naaam mpiraaaaaaa umeanza
03' Peter Banda anashindwa kuweka mpira kambani baada ya kutokea Krosi ya Kibu, ilikuwa hatari lango la Pamba FC.
05' Nafasi nyingine tena kwa simba kushindwa kuandika bao, Mhilu anakosaaaaaa.
07' Bocco na Kibu wanashindwa kutumia nafasi nzuri ya kufunga, Simba hizi nafasi watajutia kama hawatapata ushindi.
10' Yusuf Mhilu tena anashindwa kuunganisha Krosi bomba ya Banda
Pamba FC hawajapata nafasi ya kumfikia golikipa wa Simba, Beno kutokana na mashambulizi yao kuishia kwa mabeki wa Simba SC
18' Jaribio la kwanza kwa Pamba FC kwa shuti kali, lakini golikipa Beno anarukaaaa na kuokoa hatari ile na kuwa Kona ambayo haikuzaa matunda
20' Simba SC 0-0 Pamba FC
Free Kick inapigwa kuelekea Simba SC lakini golikipa Beno, anadaka bila wasiwasi, Pamba FC wameamka sasa.
23' Nafasi nyingine kwa Simba, Bocco, anakosaaaaaa kichwa cha John Bocco kinashindwa kulenga lango, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga.
28' Simba SC wamepata Kona tatu mfululizo bila mafaniko ya kufunga.
33' Salum Sheshe wa Pamba FC anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumvuta Jezi Hussein
37' Robert Makidala anakosa nafasi nzuri ya kufunga, ilikuwa Shambulizi kali kuelekea Simba | wakati huo huo Mohamed Said ameoneshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Kibu
43' Pascal Wawa anaonyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya, Pamba wanacheza eneo lao la nyuma kuwavuta Simba
45' Abdi Banda anaipatia Simba bao la kwanza
45' Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza
Mwisho wa msimu huu MkuuHmmmh, huyu kibu mbona kama kazinduka sikuhizi??
Naona anatafuta namna ya kukwepa panga la usajili, kwenye ligi ana magoli mangapi?Mwisho wa msimu huu Mkuu