FT: Biashara 0 Simba 0

FT: Biashara 0 Simba 0

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Hatimaye Siku imefika, Siku Imewadia, Kwa Miamba Miwili Ya Soka Nchi Tanzania Ambayo Inawakilisha Nchi kwenye michuano Ya Kimataifa Kukutana kwa Mtanange wa Dakika 90+ Kwenye Kipute cha Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi Isiyo Na Mdhamini.

Bado Dakika 60 Game Kuanza huku, Mashabiki Wengi Wa Simba wakiwa Wanasubiri kwa hamu kuona kikosi cha Timu yao. Wengi wakitaka kujua Je Stiker Mugalu ataanzia Benchi Au Ataanza na Kikosi cha kwanza? Baada ya kukosa Nafasi nyingi Kwenye Mchezo uliopita na Mtani wa Jadi

Tuwe hapa kwa pamoja kwa Dakika 90 za Mchezo

Here we Go…
 
Kikosi cha leo...
Screenshot_20210928-151040_Instagram.jpg
 
Asiyemtaka Mugalu, ahame Simba SC. Timu ziko nyingi, msitusumbue.

Nilisikika nikitoa angalizo mapemaaa kabla ligi haijaanza.
Anayemtaka Mugalu aende nae Congo, hatutaki wachezaji wanaobahatisha game, Simba ni timu kubwa sana! Hebu fikiria Mayele alipata nafasi moja tu ya kwanza kaitendea haki, Mugalu wetu hata kulipokuwa usiku bado anapigaga nje au kupaisha, hivi anaijua thamani yake na ya klabu ya Simba kweli??? Hapana mimi bado nna hasira aisee, akae bench tu akina Kagere na Kibu wasimamie show!
......Alisikika shabiki mmoja akifoka kwa hasira!
 
Nadhani issue yake ya uraia ndio imempa wasiwasi kocha kumpanga, mambo hayo yakishashughulikiwa tutakua tunamwona kijana.
Kocha anamuelewa sana dogo.
kweli! sema hii issue yake ya uraia imekaa vp mbona kama sielewi make ilikuwaje ile friendly match na Malawi jamaa alipewa nafasi na akacheza afu ile mechi nadhani ilkuwa inatambulika na FIFA
 
Anayemtaka Mugalu aende nae Congo, hatutaki wachezaji wanaobahatisha game, Simba ni timu kubwa sana! Hebu fikiria Mayele alipata nafasi moja tu ya kwanza kaitendea haki, Mugalu wetu hata kulipokuwa usiku bado anapigaga nje au kupaisha, hivi anaijua thamani yake na ya klabu ya Simba kweli??? Hapana mimi bado nna hasira aisee, akae bench tu akina Kagere na Kibu wasimamie show!
......Alisikika shabiki mmoja akifoka kwa hasira!
Mkuu, mwanao akifanya kosa haumkati pua wala kumvunja mguu.
Tujifunze kulinda vilivyo vyetu, Mugalu ana vitu vingi sana chanya kwa timu yetu, hata yeye hapendi kutofunga magoli. Yale ni makosa anafanya na hatutakiwi kumbomoa kupitia makosa yake.

Tunapaswa kusimama nae katika nyakati ngumu, yule ni mtu mzima anajua mashabiki tunataka nini kwake.

Katika hili, kuonyesha kwamba hatumtaki Mugalu ni utoto wa hali ya juu.
 
kweli! sema hii issue yake ya uraia imekaa vp mbona kama sielewi make ilikuwaje ile friendly match na Malawi jamaa alipewa nafasi na akacheza afu ile mechi nadhani ilkuwa inatambulika na FIFA
Jamaa inasemekana chimbuko lake ni kama anatokea maeneo ya makambi ya wakimbizi au mpakani, hivyo uraia wake una walakini. Hivyo wanataka kujiridhisha kwanza juu ya hilo na kusiwe na utata wowote. Vinginevyo nchi inaweza kuingia kwenye kashfa kubwa si unajua tena haya mambo?

That's why wanataka ku clear kabisa
 
Dah kweli! hapo nimekupata mkuu
 
Huyu mugalu hastahili hata kuwa kwenye bench LA simba
 
Back
Top Bottom