Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Heri ya Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ni jumapili tulivu, Mnyama Mkubwa Mwituni, Simba Sports atashuka dimbani dhidi ya wenyeji wake Bravos ya Angola katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Katika mchezo wa kwanza, Simba akiwa nyumbani aliibuka na ushindi wa 1-0, je ataendeleza wimbi la ushindi?
Simba inazidi kuimarika hasa ikichagizwa na ongezeko la Mpanzu, huku ikiwa nafasi ya pili na alama 9 wakati wenyeji Bravo wakiwa nafasi ya 3 na alama 6. Ni mtanange wa kufa na kupona.
Ikumbukwe kuwa Bravos ameshinda mechi zake mbili akiwa nyumbani, huku Simba akitoka kushinda ugenini mechi iliyopita, patawaka moto!
Mechi itakuwa mubashara Saa 1:00 Usiku kwa masaa ya Afrika ya Mashariki.
Karibuni wote, mshuhudie wawakilishi sahihi wa kimataifa wasiotumia CALCULATOR wakielekea Robo Fainali kama ilivyoada yao!!
================================================
1’ Simba wanaanza mpira kwa kasi kubwa
3’ ndani ya dakika hizi za mwanzoni, Mpanzu kashafanyiwa faulo mara mbili
6’ Simba wanapata kona ya kwanza
9’ Timu zote bado zinasomana
13’ Goaaaaaaaalllllllll
Bravos 1-0 Simba
15’ Simba wanaliandama lango la Bravos kama nyuki
17’ Jean Charles Ahoua anafanyiwa faulo nje ya box la Bravos
18’ Kibu anapiga lakini inakuwa nyepesi kwa kipa
21‘ FC Bravos 1-0 Simba SC
25’ Kipa wa Bravos amelala chini anapatiwa matibabu
27’ Ameamka mechi inaendelea
30’ Bravos 1-0 Simba
32’ Bravos wanakosa nafasi ya wazi ya kuongeza goli la pili
34’ Beki Che malone leo hayupo kwenye fomu yake anafanya makosa mengi sana
37’ Kibu D anapiga kichwa kikali ila mpira unaokolewa na kipa wa Bravos, mpira umechangamka
41’ Mpira wa kichwa uliopigwa na Kibu unagonga nguzo na kurejea uwanjani…
43’ Simba wana umiliki mzuri wa mpira mpaka sasa ila wanakosa utulivu wakifika golini kwa Bravos
44’ Dakika 3 za nyongeza
HT‘ FC Bravos 1-0 Simba SC
46’ Kipindi cha Pili kimeanza kwa Simba kufanya sub
Kagoma - out
Debora - in
47’ Ateba anapiga shuti kali ila mpira unapaa juu ya lango
52’ Mpanzu anatoka, Chasambi anaingia
55‘ FC Bravos 1-0 Simba SC
57’ Simba wanatengeneza mashambulizi ila wanashindwa kutumia nafasi
58’ Ngoma anapiga kichwa na kupaisha
60’ Wachezaji wa Bravos wameanza kupoteza muda sasa
67’ Atebaaaaaaaaaaa
Anasawazisha
76’ Okejepha anachukua nafasi ya Kibu D
79’ Debora Fernandez anapewa kadi ya njano baada ya kumchezea mchezaji wa Bravos madhambi
80’ Bravos 1-1 Simba Sports
85’ Bravos 1-1 Simba Sports
87’ Camara anapewa kadi ya njano kwa kupoteza muda
88’ Valentino Mashaka anachukua nafasi ya Ateba
90’ Dakika 5 za nyongeza
FT’ Bravos 1-1 Simba Sports