Heri ya Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ni jumapili tulivu, Mnyama Mkubwa Mwituni, Simba Sports atashuka dimbani dhidi ya wenyeji wake Bravos ya Angola katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Katika mchezo wa kwanza, Simba akiwa nyumbani aliibuka na ushindi wa 1-0, je ataendeleza wimbi la ushindi?
Simba inazidi kuimarika hasa ikichagizwa na ongezeko la Mpanzu, huku ikiwa nafasi ya pili na alama 9 wakati wenyeji Bravo wakiwa nafasi ya 3 na alama 6. Ni mtanange wa kufa na kupona.
Ikumbukwe kuwa Bravos ameshinda mechi zake mbili akiwa nyumbani, huku Simba akitoka kushinda ugenini mechi iliyopita, patawaka moto!
Mechi itakuwa mubashara Saa 1:00 Usiku kwa masaa ya Afrika ya Mashariki.
Karibuni wote, mshuhudie wawakilishi sahihi wa kimataifa wasiotumia CALCULATOR wakielekea Robo Fainali kama ilivyoada yao!!
View attachment 3199863
================================================
1β Simba wanaanza mpira kwa kasi kubwa
3β ndani ya dakika hizi za mwanzoni, Mpanzu kashafanyiwa faulo mara mbili
6β Simba wanapata kona ya kwanza
9β Timu zote bado zinasomana
12β Goaaaaaaaalllllllll
Bravos 1-0 Simba
15β Simba wanaliandama lango la Bravos kama nyuki
17β Jean Charles Ahoua anafanyiwa faulo nje ya box la Bravos
18β Kibu anapiga lakini inakuwa nyepesi kwa kipa
21β FC Bravos 1-0 Simba SC
25β Kipa wa Bravos amelala chini anapatiwa matibabu
27β Ameamka mechi inaendelea