FT: Bravos do Maquis 1-1 Simba SC | CAF Confederation Cup | Estadio 11 de Novembre | 12.01.2025

FT: Bravos do Maquis 1-1 Simba SC | CAF Confederation Cup | Estadio 11 de Novembre | 12.01.2025

Heri ya Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ni jumapili tulivu, Mnyama Mkubwa Mwituni, Simba Sports atashuka dimbani dhidi ya wenyeji wake Bravos ya Angola katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika mchezo wa kwanza, Simba akiwa nyumbani aliibuka na ushindi wa 1-0, je ataendeleza wimbi la ushindi?

Simba inazidi kuimarika hasa ikichagizwa na ongezeko la Mpanzu, huku ikiwa nafasi ya pili na alama 9 wakati wenyeji Bravo wakiwa nafasi ya 3 na alama 6. Ni mtanange wa kufa na kupona.

Ikumbukwe kuwa Bravos ameshinda mechi zake mbili akiwa nyumbani, huku Simba akitoka kushinda ugenini mechi iliyopita, patawaka moto!

Mechi itakuwa mubashara Saa 1:00 Usiku kwa masaa ya Afrika ya Mashariki.

Karibuni wote, mshuhudie wawakilishi sahihi wa kimataifa wasiotumia CALCULATOR wakielekea Robo Fainali kama ilivyoada yao!!

View attachment 3199863

================================================

1’ Simba wanaanza mpira kwa kasi kubwa

3’ ndani ya dakika hizi za mwanzoni, Mpanzu kashafanyiwa faulo mara mbili

6’ Simba wanapata kona ya kwanza

9’ Timu zote bado zinasomana

12’ Goaaaaaaaalllllllll
Bravos 1-0 Simba

15’ Simba wanaliandama lango la Bravos kama nyuki

17’ Jean Charles Ahoua anafanyiwa faulo nje ya box la Bravos

18’ Kibu anapiga lakini inakuwa nyepesi kwa kipa

21‘ FC Bravos 1-0 Simba SC

25’ Kipa wa Bravos amelala chini anapatiwa matibabu

27’ Ameamka mechi inaendelea
Tutashinda inshallah
 
Makolo mbn kama wameanza kupoteana ata kipind cha 2 bado maana tunajua wakirudi kipind cha 2 wanaukua unga tu 🤣
 
Mkilambwa hiii game inayo kuja mna Mwarabu afu bravo ana kibonde mshika mkia
 
Back
Top Bottom