FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

Waarabu stage hii kwao hawakuachi hata ufanyeje.

Malengo yao yametimia.
 
Imagine unaenda kwa Mwarabu, halafu anakuchezesha saa nne usiku! Na lile libaridi la usiku! Ukijumlisha na rekodi mbovu mnapocheza mechi za ugenini!

Dah! Uwezekano wa kusonga mbele, utategemea tu majaliwa ya Mwenyezi Mungu.
Gemu ina matokeo matatu, leo tumeshinda yajayo majaaliwa
 
Watu waliosababisha Simba ikose ushindi mkubwa ni kocha Kwa kuchelewa kumtoa Tibazonkiza na Chama ameharibu movie nyingi sana..

Hii Timu ilikuwa inapigwa 3=0
 
Simba hongera sana nawapenda...
Lolote litakalotokea badae nipo na nyie bega bega..
Mmeupiga mwingiiii walisema hamtawafunga waidada ila mmewafunga...
Yani kikubwa mmewafunga hilo tuu baaaaasiiiiiiii....
 
Mpira una maajabu yake ,furahia ushindi leo .

Mimi naliogopa Vibe la mashabiki wa kule mechi hizi wanashangilia kama wehu au vichaaa na wachezaji wanakuja na familia zao uwanjani kama wanapigana Jihad kutetea familia na nchi huwa hawana mzaha.
 
Sasa mjiandae kutoka maana I am sure Simba hatoweza kucheza mithili alivyocheza leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…