Leo ndiyo nngwe ya pili ya Fainali ya kombe la Shirikisho Afrika ikiikutanisha timu ya USM Alger ya nchini Algeria na Yanga SC ya Tanzania ambapo Yanga itakuwa ugenini. Katika mchezo wa kwanza Yanga ilipoteza 2-1 katika uwanja wa Benjamini Mkapa.
Timu hizi katika historia zimeingia fainali kwa mara ya kwanza, Je kutokana na ulivyouona mchezo wa kwanza unadhani mchezo huu utakuwaje?
Nani unampa nafasi ya kuibuka bingwa?
Usiku wa kuamkia mechi leo nchini Algeria Mashabiki wa USM Alger walienda nje ya Hotel waliyofikia Yanga Algeria The Legacy Luxury na kuanza kupiga mafataki, unaambiwa hii ni tabia yako kwa lengo la kuitoa mchezoni timu ya ugenini.Yanga saa 22:00 kwa saa za Tanzania leo watacheza mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikishi Afrika dhidi ya USM Alger baada ya ule wa kwanza Dar es Salaam USM Alger kuibuka kidedea 2-1.
---
Vikosi vinavyoanza leo
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha USM Alger
Bado dakika chache mtanange huu uanze, kaa hapa nami kwa upates mbalimbali.
Vikosi vimeshaingia Dimbani wa ajili ya kupasha misuli joto
---
Vikosi vimeshaingia dimbani tayari kukiwasha.
Atmosphere ya Uwanja ni hatari sana. Hawa waarabu wamepiga fataki za kufa mtu mpaka uwanja unafuka Moshi
- Mpira umeanza kwa kasi huku Yanga wakilifikia lango la Algers mapema bila kupata bao
- Yanga wanapata penati dakika ya 5 Djuma amepewa aipige
- Gooooool Yanga wanatangulia hapa...
- Timu zinashambuliana kwa zamu sasa ni dakika ya 15
- Dk 20 bado timu zinashambuliana huku umakini ukiongezeka. Yanga bado anaongoza bado Moja la Djuma Shabaan
- Dakika 35 Yanga wanasukuma mashambulizi kuelekea lango la USM Alger
- Dakika ya 39 ni Water Break hapa
- Dakika ya 45 zimekamilika zimeongezwa dakika 5 hapa
- USM Alger wanapa faulo katika eneo zuri. Diara anaokoa kwenye chaki.
- Mapumziko Yanga wanaenda wakiwa mbele ugenini