FT: CAFCC FINAL 22/23 Second Leg | USM Alger 0-1 Yanga SC 03/06/2023

FT: CAFCC FINAL 22/23 Second Leg | USM Alger 0-1 Yanga SC 03/06/2023

Usisahau kuwa hakuna team yoyote uliyowahi kuingia fainali kisha ikaanza kwa kupoteza mechi yake ya nyumabani isipokuwa Yanga.

Kuna uwezekano ikapigwa nje-ndani na kuandika record ya kipekee.
Sawa ila fainali ndio nishafika na medali nishavaa.
 
Azizi Ki hamna kitu pale, yule ni mchezaji wa msimu.

Kiwango chake hakipo constant
Alikuwa ni player wa kampeni kama ilivyokuwa kwa Manzoki Simba sc, tofauti ya Simba Sc ni kwamba hawakuingia mkenge kumsajili.
 
Leo ndiyo nngwe ya pili ya Fainali ya kombe la Shirikisho Afrika ikiikutanisha timu ya USM Alger ya nchini Algeria na Yanga SC ya Tanzania ambapo Yanga itakuwa ugenini. Katika mchezo wa kwanza Yanga ilipoteza 2-1 katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Timu hizi katika historia zimeingia fainali kwa mara ya kwanza, Je kutokana na ulivyouona mchezo wa kwanza unadhani mchezo huu utakuwaje?

Nani unampa nafasi ya kuibuka bingwa?

Usiku wa kuamkia mechi leo nchini Algeria Mashabiki wa USM Alger walienda nje ya Hotel waliyofikia Yanga Algeria The Legacy Luxury na kuanza kupiga mafataki, unaambiwa hii ni tabia yako kwa lengo la kuitoa mchezoni timu ya ugenini.Yanga saa 22:00 kwa saa za Tanzania leo watacheza mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikishi Afrika dhidi ya USM Alger baada ya ule wa kwanza Dar es Salaam USM Alger kuibuka kidedea 2-1.

View attachment 2645132
Hali ya Uwanja saa 2 kabla ya mechi
---

Vikosi vinavyoanza leo

Kikosi cha Yanga
Kikosi cha USM Alger


Bado dakika chache mtanange huu uanze, kaa hapa nami kwa upates mbalimbali.

Vikosi vimeshaingia Dimbani wa ajili ya kupasha misuli joto
---
Vikosi vimeshaingia dimbani tayari kukiwasha.

Atmosphere ya Uwanja ni hatari sana. Hawa waarabu wamepiga fataki za kufa mtu mpaka uwanja unafuka Moshi
Mvua ya mawe inakaribia kuanza
 
Imeanza.

Yanga wakishinda mbele ya mashabiki waarabu wote hawa watakuwa wametisha sana.
 
Back
Top Bottom