FT: CAFCL - Al Hilal Vs MC Algier | (1-1)

FT: CAFCL - Al Hilal Vs MC Algier | (1-1)

Caf wanaangalia head to head na sio magoli ili ufuzu inabidi umfunge al hilal 3 bila kwake halafu mc algier ukimpiga goli zozote unafuzu
Mhhh ndio maana unakuwaga mbishi. Kama Yanga akishinda mechi mbili kwa idadi yoyote ya magoli anafuzu bila matatizo na kama akidroo na Al Hilal basi mechi yake ya MC Algier anatakiwa ashinde kwa tofauti ya magoli matatu ili afuzu. Ila kundi bado lipo wazi hata kwa Mazembe, huu mpira unadunda kwa yoyote.
 
1736112764317.png
 
Al hilal anacheza na yanga kabla ya kukutana na mazembe.

Al hilal hawezi kukubali kumaliza nafasi ya pili ili akutane na al ahly au esperance atataka amalize wa kwanza apate unafuu
Yaani ndiyo nimeangalia hapa ratiba nimegundua hilo. Hii sasa ni tamu kuliko hata embe lililoiva 🤣😂🤣

Halafu kama sikosei kimahesabu hata Mazembe bado ana nafasi ya kufuzu!
 
Usipende kukatiza mada bila kujua kinachoongelewa. Uliona wapi mmoja ana point 8 mwingine ana point 10 halafu achukuliwe mwenye point 8 kisa head to head? Pitia comments za juu kabla ya kujibu ili ujue kinachoongelewa
Nakufundisha mpira bila ada kama mc alger angeshinda ilitakiwa umfunge al hilal halafu mechi ya mwisho umfunge goli 3 bila mc alger ili uwe juu yake kwenye head to head hapa na assume mc alger kampiga mazembe kumbuka nili ku quote wakati mc alger anaongoza bado hajasawazishiwa
 
Mhhh ndio maana unakuwaga mbishi. Kama Yanga akishinda mechi mbili kwa idadi yoyote ya magoli anafuzu bila matatizo. Ila kama akidroo na Al Hilal basi mechi yake ya MC Algier anatakiwa ashinde kwa tofauti ya magoli matatu. Ila kundi bado lipo wazi hata kwa Mazembe, huu mpira unadunda kwa yoyote.
Sorry hapo nilikosea nilimaanisha mc alger na sio al hilal
 
Wa kuanza kujicheka ni ninyi wenyewe simba bado wana nafasi ninyi hapo mlipo mnategemea mazembe akawaokoe kule algeria, hivi kwa akili ya kawaida tu mnaona hilo linawezekana kweli ninyi kwa al hilal lazima mgongeke na mazembe nao kule algeria lazima wagongeke, kwahiyo ninyi hata mkimfunga muarabu hapa hamtoboi sana sana mtajifariji tu kuwa walau hamjaishia makundi mkiwa mnaburuza mkia
Nimechukua risiti ndugu yangu 😃 😀
 
Caf wanaangalia head to head na sio magoli. Yanga ili afuzu inabidi amfunge al hilal 3 bila.
H2H inayoangaliwa ni pindi timu mbili zilizofungana pointi

H2H itawahusu wao kwa wao walivyokutana na sio magoli ambayo yamefungwa kwenye mechi zingine.

Hiyi ya magoli ya mechi zingine itakuja baada ya wao kwa wao kuonesha wame balance kwenye magoli. Japo magoli yaliyofungwa ugenini pia yanaweza kuamua.
 
Al hilal ameshafuzu tayari... Kwenye hili kundi ni Yanga na Mc A. ndio wanaweza kufikisha point 10. Lakini wanakutana wao kwa wao hivyo matokeo yoyote yale hayatamuathiri Al hilal. Maana haiwezekani wote wakafikisha point 10.
 
Maanake nafasi ya pili bado ipo wazi, match day 5 inaenda kutoa mwanga ila Yanga imepata ahueni wanatakiwa wakapambane haswa mechi inayofuata amfunge Al Hilal
Huo mfupa wa kumfunga Al Hilaly nyumbani kwake, ni mgumu sana kwa Yanga. Akijitahidi sana ni droo
 
Kwenye mechi mbili Simba kutafuta point 1 ni hali ngumu?

Kama mwenye point 9 ana hali ngumu vipi mwenye point 4 hali yake ipoje?
Mwenye 4 ana ari, nguvu na uwezo. Huyu mwenye 9 anabangaiza na kubahatisha.

Usiniulize kama ana ari, nguvu na uwezo kwann ana 4? Jibu ni kwamba gari lake lilichelewa kuwaka.

Hivi sasa hata Real Madrid anapigwa mkono
 
Mwenye 4 ana ari, nguvu na uwezo. Huyu mwenye 9 anabangaiza na kubahatisha.

Usiniulize kama ana ari, nguvu na uwezo kwann ana 4? Jibu ni kwamba gari lake lilichelewa kuwaka.

Hivi sasa hata Real Madrid anapigwa mkono
Umenikumbusha mbali sana, kauli zinafanana na zile za kipindi hichooo za mfalme mmoja hivi akiitwa mfalme Juha🤣🤣🤣
 
Kifupi Al Hilal anaweza asiendelee mbele kama atakubali kufungwa leo.
Yanga ana point 4 mechi mbili mkononi!
Akimpiga Al Hilal na MC Algiers.
Ana uhakika.
Yaani unasema Al hilal hawezi pata point kwa mazembe?
 
Back
Top Bottom