FT: CAFCL: Mamelodi Sundowns 2-2 Wydad Casablanca | Live Updates | Mei 20, 2023

FT: CAFCL: Mamelodi Sundowns 2-2 Wydad Casablanca | Live Updates | Mei 20, 2023

Scars

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
48,055
Reaction score
116,512
Mchezo huu ni wa Nusu Fainali ya pili baina ya timu hizo katika Ligi ya Mabingwa Afrika, unapigwa Nchini Afrika Kusini baada ya awali kumalizika kwa suluhu ya 0-0 Nchini Morocco.

Mchezo umeanza

20' Mamelodi Sundowns wanafanya mashambulizi kadhaa, wageni nao wanajibu lakini bado hakuna umakini langoni

Kumbuka kuwa timu itakayofanikiwa kusonga mbele itakutana na Al Ahly katika mchezo wa Fainali itakayofanyika mwezi ujao

45' Mapumziko hakuna timu iliyopata goli

Half time.JPG

Kipindi cha pili kimeanza

Goooooooooooooo
50' Themba Zwane anafunga goli baada ya wachezaji wa Wydad kujichanganya
Kipa alirusha mpira uliombabatiza beki wake, jamaa wakatumia fursa
53' Mamelodi wanaongeza presha kubwa kutafuta goli la pili
65' Wydad wanafanya shambulizi kali lakini mpira unaokolewa na kuwa kona
69' Kasi ya mchezo imepungua kiasi fulani hasa baada ya wenyeji kupata goli
70' Wydad wanafanya shambulizi lingine kali, mashuti mawili yanaokolewa inakuwa kona
GOOOOOOOOOOOOOOOOO
Ni kama ilikuwa linakuja kutokana na wenyeji kuruhusu kushambuliwa mara kwa mara
72' Ayoub El Amloud anawapatia goli wageni, matokeo ni 1-1
79' GOOOOOOOOOOOOOOOOO
Peter Shalulile anafunga goli la pili kwa Mamelodi
83' Gooooooooooooooooo
Mothobi Mvala anajifunga kwa kichwa wakati akitaka kuokoa mpira wa faulo

FULL TIME

Wydad imesonga mbele kwa faida ya goli la ugenini baada ya awali timu hizo kutoka 0-0 Nchini Morocco.
 
09'
Mamelody wanashambulia goli la Wydad
 
11'
Wydad wanajaribu kufika kwenye eneo la Mamelody lakini wanazuiwa
 
14'
Mchezaji wa Mamelody anapiga shuti lakini mlimda mlango anadaka
 
15'
Eneo lile lile tena mchezaji anafanya jaribio la kufunga lakini golikipa wa Wydad anaudaka mpira
 
19'
Wydad wanafanya shambulizi la kushtukiza hapa ulipogwa mpira mrefu kumtafuta mshambuliaji ambaye alikuwa anakimbuzana na defender lakini mlinda mlango wa Mamelody aliwahi kuunusuru mpira
 
21'
Mamelody wanakosa bao hapa baada ya one two kukubali mpira ulipigwa kipa akautema, beki wa Wydad akaamua kuutoa nje na kuwa kona
 
22'
Mamelody wanapata kona ya kwanza hapa
 
23'
Mamelody wanakosa nafasi ya wazi hapa
 
Back
Top Bottom