Mechi imeisha kama nilivyotabiri.
Kumbukeni Yanga hawezi kumfunga CRB kwa tofauti ya goli 3 (na wakifanya mchezo wanaweza kupoteza vile vile). Wakisema wacheze kwa kuzitafuta goli nyingi, pakacha la kina Mwamnyeto nalo litakuwa linavuja.
Kwa maana hiyo hata akimfunga katika mechi ijayo, CRB bado ana uhakika wa kumfunga Medeama mechi ya mwisho. Yanga hawezi kumfunga Al Ahly kwao katika mechi ya mwisho, hilo haliwezi kutokea.
Kwa hiyo, baada ya mechi za mwisho hata Yanga na CRB wakilingana points, wataangalia kwanza walivyokutana aggregate inasomaje.
Hayo ndiyo mahesabu.