FT: CS Sfaxien FC 0-1 Simba SC | CAF CC | Stade Olympique Hammadi Agrebi | 05.01.2025

FT: CS Sfaxien FC 0-1 Simba SC | CAF CC | Stade Olympique Hammadi Agrebi | 05.01.2025

Tembosa

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,487
Reaction score
3,978
Siku ya Mechi Kali.
20250105_172017.jpg

Screenshot_20250105-154843~2.png


Mwenyeji: CS Sfaxien FC

Mgeni : Simba SC

Mashindano: CAF CC Group Stage.
Group A.

Uwanja: Stade Olympique Hammadi Agrebi Stadium, Rades, Tunisia.

Tarehe: 05th January 2025

Muda: Saa 1Jioni (EAT)

VIKOSI.
1. CS Sfaxien

2. Simba SC
20250105_180809.jpg



Updates On 1st Half

00' Mpira Umeanza hapa kwa kasi, Simba wamechezewa Faulo

03' SC Sfaxien wanafanya shambulizi anaokoa Camara, wakati huo anaenda chini baada ya kuchezewa Rafu na Sfaxien
Game On
0-0

05' Sfaxien wanapata free kick nje kidogo ya 18 inapigwa inagonga mtambaa panya, inakuwa offside.
0-0

10' Mpira unaendelea Ngoma anachezewa faulo katikati ya uwanja.
Inapigwa wanatengeneza shambulizi linakuwa hafifu.
Game On
0-0

13' Simba wanapata kona ya kwanza, inaondoshwa kirahisi sana.

17' Wanacheza Free Kick Sfaxien inapigwa Che Fondo Malone anaitoa kwa ustadi mkubwa kabisa.
Game On
0-0

23' Ahoua anachezewa rafu mbaya kidogo, haimuumizi mpira unaendelea sasa
0-0

26' Simba wanapata kona ya pili inapigwa na Jean Charles Ahoua inatolewa inakuwa goal kick.
Game On
0-0

27' Elia Mpanzu anapatiwa kadi ya Njano baada yakucheza faulo.
0-0

31' Ateba amechezewa vibaya hapa, imekua faulo. mpira unaendelea
0-0

33' Goooooooooooal Chumaaaaaa kituuuuuuuuuuuu.
Jean Charles Ahoua anapiga kitu cha moto Sfaxien wanakandwa hapa, wanapigwa msumari.
Ilianza kwa Che Malone Ikapigwa kwa Ateba akaitoa kwa ustadi mkubwa sana Ikamfikia Ahoua akatupia.
0-1

36' Simba wanapata kona nyingine inapigwa inakatalia.
Simba wanaumiliki sana Mpira wanacheza mpira
0-1

39' Simba wanapata kona nyingine inapigwa inaishia kwenye mikono ya kipa wa Sfaxien
Game On
0-1

44' Sfaxien wanapata free kick nje kidogo ya 18.
Inapigwa inaokolewa.

45' Nyongeza ni 1' tu.
0-1

45+1' Ateba anapewa kadi ya Njano.
Baada ya kwenda kumzuia Mchezaji wa Sfaxien asianzishe Mpira.

HALF TIME
SC Sfaxien 0-1 Simba
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Kipindi Cha Pili.
Updates
45' Mpira umeanza hapa kwa ajili ya 2nd Half.
0-1

49' Simba wanapata free kick nje kidogo ya 18, inapigwa free kick ya maana sana hapa.
Inakuwa kona.
Simba wanapata kona nyingine hapa.
Inapigwa inaondoshwa hapa.
Game On
0-1

51' Sfaxien wanapata free kick hapa baada ya Ngoma F kucheza faulo.
inapigwa haileti madhara yoyote kwenye lango la Simba.
0-1

53' Sfaxien wanapata free kick wanapiga inapitiliza nje.
Goal kick
Game On
0-1

58' Sfaxien wanafanya mabadiliko mawili
Mpanzu anapiga cross moja inatolewa kwa kichwa.
Inakuwa kona inapigwa inatolewa
Mpira unaendelea
0-1

60' Sfaxien wamejaribu kufanya kaunta attack hapa, Camara anaitokea na kuokoa.
Mpira umesimama hapa Camara anapatiwa matibabu baada yakugongana na mchezaji wa Sfaxien.
0-1

76' Simba wanafanya mabadiliko
Eli Mpanzu Out
Deborah Fernandez Inn
Game On
0-1

83' Sfaxien wanapata free kick nje inapigwa vizuri wanajichanganya wanapoteza nafasi ya wazi kabisa. hapa Sfaxien
Game On
0-1

86' Substitute kwa Simba
Kibu Out
Chamoue Inn
Game On
0-1

89' Sfaxien wanapata kona, inapigwa inakuwa butu.
Simba Substitution
Ateba Out
Mukwala Inn

90' nyongeza ni 5'
Game On
0-1

90+5' Mpira Umekwisha.

Sfaxien 0 - 1 Simba
 
Guvu Moyaaaa!!
Mpira ulichezwa jana! Leo tuna hangover sidhani kama tutaona vizuri.
Marefa hawatahongeka huko ni kichapo tu leo. Simba ikipata droo mniite!!
Lolote liwakute kolowizards!!
 
Nawatakia kipigo chema mbu watatu(mbu mbu mbu).

RAGE MUNGU ANAKUONA, ULITUMIA KIGEZO GANI MAKOLO WOTE KUWALINGANISHA NA MBU WATATU?

kama upo humu, tafadhali nijibu.
 
Back
Top Bottom