FT: Geita Gold FC 0 - 3 Yanga SC | NBC League | CCM Kirumba Mwanza | Oktoba 7, 2023

FT: Geita Gold FC 0 - 3 Yanga SC | NBC League | CCM Kirumba Mwanza | Oktoba 7, 2023

Nguvu kubwa itatumika nje ya dk 90 ili YANGA washinde.
 
Yule refa wao aliewapa penati hayupo,kipigo kitawahusu wana wa utopolo
 
Hello wanamichezo wote Jf!?
I hope mko poa mkiendelea na majukumu yenu mbalimbali.... Najua wengine hawapo poa kutokana na magonjwa au matatizo mbalimbali ya dunia hii, usife moyo Bali mtangulize Mungu Kwa kila Jambo.

Leo bingwa mtetezi wa ligi namba tano Kwa Ubora barani Afrika namaanisha NBC PREMIER LEAGUE, Dar Young Africans maarufu kama Yanga SC itakua mgeni wa Geita Gold FC Katika dimba la CCM Kirumba pale Jiji la Sato na sangara.

Huu utakua mchezo wa tano Kwa Yanga ambaye ana points 9 akiwa nafasi ya tatu nyuma ya Kinara Azam FC na Simba SC. Yanga baada ya kupokea kichapo cha 2-1 kutoka Kwa Ihefu FC Leo atapambana kushinda ili kurejesha furaha Kwa mashabiki wao Ambao wamepitia kipindi kigumu wiki hii kutoka Kwa watani zao Simba. Kwa upande wa Geita Gold FC wao wapo nafasi ya 12 wakiwa na points 4 hivo watapambana walau wapate sare ili watoke nafasi za hatari.

Katika mechi 4 walizokuatana, Yanga kashinda mechi zote nne hivo ana rekodi nzuri. Mechi ya mwisho kukutana Yanga walishinda Bao tatu zilizopachikwa na Mzize, Musonda na Jesus Moloko Bao pekee la Geita Gold lilifungwa na Fundi Elias Maguli Je, Yanga wataendeleza utabe wao au Geita Gold FC watafuta uteja?

Kwa hayo na mengine mengi, Basi andaa macho na masikio leo saa 10:00 jioni katika dimba la CCM KIRUMBA pale Ilemela Mwanza Moto Utawaka. Updates zote utazipata kupitia huu Uzi..

Kila la kheri Wanachi [emoji169][emoji172]
#DaimambelenyumamwikoView attachment 2774247
All the Best Yanga.
Piga hao Geita gold Goli 6
 
Naitakia ushindi Yanga. Ila kwa leo watanisamehe. Sitaangalia hiyo mechi. Matokeo nitayapata hapa hapa jukwaa la michezo.
Jikaze kiume mtani!!!

Yanga tangu aondoke Mzee wa mitetemo hata mkishinda hamna furaha.

Ila si mnao wazairwaa wengine? Watawaletea staili nyingine ya kushangilia.
 
Jikaze kiume mtani!!!

Yanga tangu aondoke Mzee wa mitetemo hata mkishinda hamna furaha.
Ila si mnao wazairwaa wengine? Watawaletea staili nyingine ya kushangilia.
Ila Mayele alikuwa ni fighter sana. Ngoja nikione kikosi kwanza. Akipanga kama kile cha mechi na Ihefu, aisee bora niende tu shamba nikaangua madafu nile.
 
Back
Top Bottom