FT|| Horoya AC 1-0 Simba SC | CAF Champions League | Stade General Lansana Conte | 11.02.2023

FT|| Horoya AC 1-0 Simba SC | CAF Champions League | Stade General Lansana Conte | 11.02.2023

Ni lazima tukubali udhaifu wetu kwenye mipira ya kutenga, hatutakiwi kuruhusu kona nyingi golini kwetu wala faulo karibu na eneo letu la hatari.

Lakini kwa ujinga ninauona leo kwa hawa mabeki wetu (hasa Onyango na Kapombe), muda sio mrefu tutawaka.
Nimesema hapa, kisha baada ya muda kidogo tu mambo yamejipa.

Kama tutaendelea kuruhusu kona za kila mara, tutakufa zaidi ya goli 3.
 
Ni msimu mwingine wa Ligi ya Mabingwa Africa. Leo hapa nyumbani Tanzania ni sikukuu kwa wapenda kandanda hasa soka la kuvutia, Samba Loketo.

Wawakilishi wa Tanzania, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC leo majira ya saa 1:00 usiku atashuka dimbani huko nchini Guinea, kuchuana na Horoya AC katika dimba la Stade General Lansana Conte.

Simba ambao wamejizolea umaarufu linapokuja suala la mechi za kimataifa, wamekuwa wakifanya vizuri sana watashuka dimbani wakiwa na lengo la kupata matokeo mazuri hasa baada ya vinara wa kundi lao Raja kuibomoa Vipers 5-0 katika mchezo uliopigwa jana usiku.

Simba itawakosa baadhi ya wachezaji kama Jonas Mkude, Augustine Okrah, Saido Ntibazonkiza ambao wamebaki nyumbani Tanzania kutokana na sababu mbalimbali.

Mchezo utakuwa mubashara kupitia ZBC2 katika Kisimbuzi cha AzamTv na Chaneli 229 katika kisimbuzi cha DStv.

Karibuni sana kwa live updates...kila la heri kwa mnyama mkubwa mwituni
View attachment 2513148
Simba inafungwa goli la kijingaa... Hovyo kabisaa ..
 
Linapokuja swala la TAIFA hua napenda kuwa mtanzania ila nkikumbuka kejeli za bob nani yule aaah
 
Safi sana wameyatungua maana yana enjoy kujizungusha zungusha nyuma,mbele hayaendi na yanacheza kama vile underdog..

Tandika mengine Horoya
 
Back
Top Bottom