FT: Ihefu FC 0-2 Simba Sc | NBC Premier League | Highland Estates Stadium | 10.04.2023

FT: Ihefu FC 0-2 Simba Sc | NBC Premier League | Highland Estates Stadium | 10.04.2023

Haya ngoja tuone freekick yao kama itazaa matunda
 
Muamala usome huko, ubao ubadilike dakika nyingi sana zimepotea... mngewahisha sasa hivi zingekuwa 6 kuelekea 7... nitarudi muamala ukisoma vizuri.
 
Majira ya Saa 10:00 Alasiri kwa masaa ya Afrika Mashariki, Ihefu Fc itawakaribisha Simba Sc katika dimba lao la Highland Estates katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Habari kubwa leo, nani wa kumzuia Jean Baleke ambaye amekuwa hazuiliki sasa, kwa taarifa yako Baleke kwasasa anafunga kila mechi, alifunga mecho iliyopita hat trick na atafunga leo na mechi ijayo atafunga kama ilivyoada.

Ihefu iliyopo nafasi ya 8 itajaribu kulipa kisasi baada ya kufanyiwa mauaji ya Sharubela juzi dhidi ya Mnyama mkubwa mwituni, Simba SC, Ihefu aliloa mabao 4-1.

Simba iliyopo nafasi ya pili, itajaribu kupunguza alama dhidi ya Yanga wanaoongoza ligi kwa tofauti ya alama 8 huku ikisalia michezo sita kabla ya ligi kutamatika.

Ewe mwanasimba uliyepo Dodoma, Nakuru, Bukoba, Mwanakwerekwe, Jinja, Eldoret, Kivu na maeneo mengine usipitwe na mchezo huu mtamu.

Mchezo utakuwa mubashara Azam Sports 1HD na tutakuletea updates hapa JamiiForums kupitia uzi huu...

View attachment 2583336

Mchezo umeanza
2' Wenyeji wanamiliki mpira muda mwingi
8' Bado Ihefu wanaonekana kuwa na nguvu zaidi kuliko Simba
16' Simba wanafanya shambulizi kali, Baleke anapaisha mpira juu licha ya kufanya kazi nzuri ya kuwatoka walinzi
19' Shuti la Sakho linatoka nje kidogo ya lango
21' Mabadiliko kwa Simba, Sawadogo anatoka, anaingia Kapama,
SIMBA itabaki kuwa kileleni
 
Back
Top Bottom