FT | Ihefu SC 1 - 1 Simba SC | NBC Premier League | Liti stadium | Aprili 13, 2024

baba aura

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2023
Posts
254
Reaction score
393
Ihefu sc vs Simba sc saa 10:00 jioni CCM Liti stadium NBC premier league
Leo wanasingida watakuwa wanashudia mtanange mkali baina ya mwenyeji ihefu vs simba sc, wakiendelea kusaka pointi muhimu za kuamua nani bingwa msimu huu.

Tukutane hapa kwa update.

KIKOSI CHA SIMBA


KIKOSI CHA IHEFU


 
Kutolewa robo kulinifurahisha. Kufirumushwa FA na mashujaa kulinifurahisha zaidi. Leo napenda tushinde ili kupunguza kelele kuelekea tar 20. Then tar 20 naombea mtani atupige walau goli moja tu. Unaijua kwanini?
Baada hapo mashabiki watasusa kwenda viwanjani, Naamini akili za viongozi wa Simba zitaamka na watakuwa makini kwenye kufanya maboresho ya timu.
 
Kuna tatizo kubwa pale Simba hivyo yanga wanaweza kucheza na mechi zetu kirahisi sana.Hakuna udhibiti wa wachezaji,hivyo mnavyoona hawajitumi,inaweza kuwa tayari mdudu kaingia kwa wachezaji.
Na hatari ni mechi ya tarehe 20.
Kuna historia inaenda kutengenezwa na Yanga.
Kitu kinachoudhi,yanga anateseka kuzifunga timu ndogo hata zinazokaribia kushuka daraja,lakini akicheza na simba ni kama anacheza na timu ya daraja la nne.Anajipangia tu afunge goli ngapi

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 

Tusiposhinda hii game, Tumelogwa.

All the Best Mnyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…