FT: Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) Simba SC 3-0 Dodoma Jiji FC | Uwanja wa Mkapa

FT: Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) Simba SC 3-0 Dodoma Jiji FC | Uwanja wa Mkapa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC), hatua ya robo fainali, kupigwa leo Jumatano ya Mei 26, 2021 ambapo Mabingwa Watetezi Simba SC, wanawakaribisha Dodoma Jiji FC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo unatazamiwa kuwa mkali sana kwa kila timu kuhitaji ushindi ili kuweza kutinga nusu fainali? Usikose Ukasimuliwa.

Kumbuka mchezo huu wa ASFC ni kuanzia majira ya saa 1:00 Usiku.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

=========

Wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Benjamin Mkapa

Naaaam mpira umeanza kombe la ASFC

Simba SC 0-0 Dodoma Jiji FC

10' Shutiiiiii kali la Miquissone linadakwa na golikipa Kalambo, ilikuwa nafasi nzuri kwa Simba SC na salama wa Dodoma Jiji

15' Hoza anapiga shuti la mbali na kutoka Sentimita chache ya lango la Simba SC

Simba SC 0-0 Dodoma Jiji FC

Justine anamuangusha Morrison eneo la 18 na refa anaamuru mkwaju wa penalty.

23' Bocco Goooooooooaaal

John Bocco anaipatia Simba SC bao la kwanza kwa mkwaju wa penalty

Simba SC 1-0 Dodoma Jiji FC

Free Kick kuelekea Simba SC, anapiga Ambundooooo lakini golikipa Manula anapangua na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda

41' Bocco Goooooooooooooaaal

John Bocco anahesabu bao la pili kwa Simba SC

Simba SC 2-0 Dodoma Jiji FC

45+2' Linapigwa Biriani hapa uwanja wa Mkapa kuelekea kuwa mapumziko

Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wapo mbele kwa mabao mawili kwa bila dhidi ya Dodoma Jiji

HT, ASFC | Simba SC 2-0 Dodoma Jiji

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa, mchezo umeanza kwa kasi kama kipindi cha cha kwanza

50' Dodoma Jiji wanasogea lango la Simba Linapigwa shutiiiiii loooooo golikipa Manula anaruka kuokoa hatari ile, lilikuwa jaribio nzuri kwa Dodoma Jiji

79' Wanakwenda sasa Simba kwake Kagere, lango la Dodoma Jiji lipo hatariniiiii
Goooooooooaaal Goooooooaaal

Maddie Kagere anaipatia Simba SC bao la tatu

Simba SC 3-0 Dodoma Jiji FC

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo, Simba wanapanga mashambulizi kwake Kagereeee anapiga shutiiiiii loooooo

Anakosa nafasi ya kufunga, golikipa Kalambo anaruka juu nakupangua mpira ule.

Biriani sasa, kwake Bwalya, kwake Duchu, mbele kuleeeee kumtafuta Morrison unatupwa pembeni kuleee kwake Mzamir

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao matatu kwa bila na kutinga nusu fainali dhidi ya Dodoma Jiji FC.

FT, ASFC | Simba SC 3-0 Dodoma Jiji FC.

...... Ghazwat
 
Manula
Kameta Kennedy Wawa Hussein
Lwanga Bwalya
Miquissone Chama Morrison
Bocco

20210526_172052.jpg
 
DODOMA JIJI FC WADAI KUNA DAWA KALI VYUMBANI [emoji3]
“ Chumba chetu cha kubadilishia nguo hapa katika uwanja wa Mkapa kimepuliziwa dawa na kuna harufu kali sana ya dawa hivyo tumemwagia maji ili kuikata na wachezaji tumewatafutia chumba kingine cha kupumzika kwa muda.

Match kamishna pamoja na daktari wa mchezo wamejiridhisha na hilo hivyo wachezaji wetu hawataingia vyumbani.” - mwisho wa kunukuu.
 
Wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Benjamin Mkapa

Naaaam mpira umeanza kombe la ASFC

Simba SC 0-0 Dodoma Jiji FC
 
Back
Top Bottom