FT: Ligi Kuu Bara | Geita Gold FC 1-1 Simba SC | Uwanja wa CCM Kirumba | Leo Mei 22, 2022

FT: Ligi Kuu Bara | Geita Gold FC 1-1 Simba SC | Uwanja wa CCM Kirumba | Leo Mei 22, 2022

Sikujua kama una akili ndogo hivi anyways nguvu moja
Huyu jamaa mechi za Simba kaingia zote

Takwimu zinaonesha kocha Nabi kaingia kuangalia mechi nyingi za simba kuzidi wale mashabiki kindaki ndaki wa tawi la chalinze

Unajua kwasababu gani amekuwa interested sana na mechi za Simba

Ngoja nikupe sababu

Unakumbuka msimu unavyoanza alikuwa na mwanzo mgumu kila time timu yake ilikuwa inapoteza kila mechi

Nabi aliwekewa vikao nyomi kama ana solve msala wa kufilisi benki, nakumhuka moja ya utetezi wake alikuwa akisema hawa wachezaji mliosajili hawakuwa kwenye chaguo langu hivyo itanihitaji siku nyingi mpaka kuwaweka kwenye muunganiko

Club ikakosa subra mpaka kufikia hatua uongozi ukampa mechi mbili za mwisho ambazo kati ya hizo akipoteza basi wanaachana naye.

Mechi hizo mbili ilikuwa ni ile ya wale wa nigeria ambayo ilikuwa ni marudiano wakiwa ugenini ambapo walipasuka bao 2

Ikabaki moja ambayo ilikuwa ni derby

Sasa simba walijawa na huruma wakaona sio vyema jamaa apoteze kibarua wakaamua kumstiri kwa kumpa fursa afunge bao moja ili aendelee kusalia jangwani.

Tangu hapo jamaa amekuwa na mapenzi makubwa mno na club ya simba, na kuna siri moja nawatobolea leo muijue.

Huyu sio mechi tu, hata kwenye mazoezi ya simba huwa anaendaga

Afu sasa anavyomkubali bocco yani usipime, ile juzi alishindwa kudhibiti hisia zake, bocco alivyofunga ikabidi aruke na kuanza kushangilia.
 
Back
Top Bottom