FT: Ligi Kuu Bara | KMC FC 1-3 Simba SC | Uwanja wa CCM Kirumba 26/12/2022

Mbona leo ni kama wana simba tunaenda kubeba droo nyingine?
 
Nyie endeleeni kuchambua mkataba wa Fei sisi ngoja tuwachambulie mechi yenu hii ya leo.
 
S

Si ulisema unahamia Jukwaaa la mapenzi?? GENTAMYCINE akishinda?
Kwani ameshatangazwa mshindi?

Atakapo tangazwa tu, nitawasiliana mara moja na mwanasheria wangu mbobevu na mwandishi nguli wa habari ndugu Pascal Mayalla, ili nione athari zitakazo jitokeza baada tu ya mimi Tate Mkuu kuhamia jukwaa la MMU.

Na kama atanisbauri niendelee kubaki huku, basi sitakuwa na namna nyingine.
 
Hamna cha kutangazwa tayari matokeo yameshajionyesha pale...huyo usiemtaka ndo mshindi
 
00' Naaaaaam mpira umeanza Uwanja wa CCM de Kirumba

KMC FC 0-0 Simba SC
 
Hamna cha kutangazwa tayari matokeo yameshajionyesha pale...huyo usiemtaka ndo mshindi
Kwa hiyo na wewe umekubali matokeo hata kabla ya mshindi kutangazwa!!

Kumbe nilikuwa sahihi kabisa kugomea mchakato mzima. Yaani mgombea unakubali kirahisi tu kushindwa!!
 
Ni wakati wa TFF kuwapa Onyo Hawa Wadhamini wanao Haribu Mpira, Hii sio Quality ya Live Video ya Mwaka 2022 ni Mateso kwa Watazamaji
 
06' Mchezo unaendelea huku kila timu ikijaribu kutafuta bao la kwanza kwa mashambulizi kadhaa pande zote.
 
Hii perfomance sio ya Simba tunayoijua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…