FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 1-0 Namungo FC | Stade de Benjamin Mkapa 16/11/2022

FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 1-0 Namungo FC | Stade de Benjamin Mkapa 16/11/2022

90+2' Kuelekea kumalizika kwa mchezo

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Namungo FC

FT: Simba SC 1-0 Namungo FC
 
Andika kama mwanaume sio kucheka cheka. Mtu akifanya vizuri atasifiwa akiboronga atasemwa. Hata hiyo akili ya kujua jambo dogo kama hilo huna?
Hajawahi kujua, hamna cha kufanya vizuri wala vibaya, Kibu ni mchezaji asiye na akili ya mpira bali nguvu nyingi zisizo na impact.

Na kuhusu kuandika, tusipangiane, naandika nitakavyo mimi sio utakavyo wewe.
 
Mh hii simba utamaliza nafasi ya 3 au ya 4 msimu huu!!!
Simba tukimaliza runner up ni jambo lakushukuru aisee tuna mizigo mingi sana kwenye timu.hata champions league nawasi wasi tukaharibu records zetu zakufanya vizuri wacha tuone
 
Kama si Mbiringe bila shaka ni Patashika ya Ligi Kuu Tanzani Bara [emoji1241] kuendelea kupigwa leo Novemba 16, 2022. Mnyama Mkali Mwituni Simba SC [emoji881] kukiwasha na Wababe wa Kusini Namungo FC, katika Uwanja wa Stade de Benjamin Mkapa Dar es salaam [emoji2522]

Mchezo unatarajiwa kuwa ngumu kwa pande zote mbili kulingana na maandalizi na ubora wa vikosi vyao huku makocha wote wakisema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo. Kocha Mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda amesema kuwa maandalizi ya mchezo yapo vizuri.

"Kwa ujumla ni kwamba maandalizi ya mchezo wa leo yanakwenda vizuri, kwa maana kuwa tupo tayari kucheza mchezo wetu na mpinzani wetu kutoka Lindi". alisema Kocha Mgunda.

Naye Kocha Msaidizi wa Namungo FC Shadrack Nsajigwa kuelekea kwenye mchezo huo amesema kuwa wamejiandaa kushindana na Simba SC.

"Kimsingi tumekuja kushindana na Simba SC, tumepata muda wa kujiandaa kiasi cha siku 8 kwahivyo timu yetu ipo tayari kwa ajili ya kushindana na Simba SC". amesema Kocha Shadrack.

Tutegemee kuona ushindani wa kweli ndani ya dakika 90 za jasho na damu kutoka pande zote mbili katika kugombea alama tatu muhimu za Ligi Kuu Tanzania Bara..[emoji288]Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1;00[emoji354] Usiku.. Usikose Ukaadithiwa Yaani.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.[emoji2424][/B]

=====================

Wachezaji wa Timu zote mbili wapo uwanjani wakipasha misuli moto tayari kwa mchezo..!

00' Naaam mpira umeanza | Simba SC 0-0 Namungo FC

02' Simba wanapata Kona ambayo haikuzaa bao.. Inaokolewa na Namungo FC

09' Simba wanafanya mashambulizi mawili ya kasi, moja Kibu akishindwa kufunga bao la kichwa huku mpira wa Kichwa wa Henock ukigonga Mlingoti

15' Dakika hizi za mwanzo Simba SC wameweza kumiliki mchezo kwa mashambulizi kadhaa

Namungo wanafanya shambulizi lakini Onyango anatokea na kucheza mpira na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

23' Kanoute anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango la Namungo FC.

25' Pasi nzuri ya Kichuya, Namungo FC wanashindwa kufunga bao..!

31' [emoji460] Phiri Goooooooooooooaaal gooal
Moses Phiri anahesabu bao la kwanza akipokea V' pasi murua kutoka kwa Hussein

35' Asante anapiga shutii la chini chini lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick.

40' Kikoti kwake Masawe mbele kuleee lakini wanapoteza mpira ule.

Kichuya anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Hussein

Sakho anapiga shutii la chini chini lakini golikipa Munishi anaruka na anadaka.

43' Namungo FC wanapata Free Kick, unapigwa mpira mrefu na kutoka nje ya lango.

45+1' Kuelekea kuwa mapumziko Uwanja wa Benjamin Mkapa

Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wapo mbele ya bao moja kwa bila dhidi ya Namungo FC

HT: Simba SC 1-0 Namungo FC

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa.. Hakuna mabadiliko kwa wachezaji wa Timu zote mbili

49' Magingi anapiga kichwa lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick

52' Sakho yupo chini akipatiwa matibabu baada kuchezewa vibaya, ameinuka mpira unaendelea

Simba wanashindwa kuifungua ngome ya Namungo, Phiri na Mzamiru walikuwa na nafasi nzuri ya kufunga.

59' Masawe anashindwa kuunganisha mpira wa Krosi kutoka kwa Kichuya

Manyanya anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Hussein

62' Kichuya na Kikoti wametoka na wameingia Mohamed Issa na Lusajo

Phiri yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kupata rabsha.. Mpira upo mbele kuleee kwake Lusajo

68' Mohamed Issa anaonyeshwa Kadi ya Njano baada ya kumchezea madhambi Kanoute

Kassim ameingia kuchukua nafasi ya Masawe, upande wa Namungo FC

75' Namungo FC wamemka kwa sasa kutafuta bao la kusawazisha, wanamiliki mpira.

78' Ametoka Okrah na ameingia Akpan huku Simba wakifanya majaribio kadhaa

Ni Free Kick kuelekea Simba eneo karibu na box la 18, Akpan anafanya faulo.. Inapigwa mpira unababatiza mabeki wa Simba

Asante anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Kibu

85' Simba wanaweka bao lakini Refa anakataa anasema ni Offside

88' Lusajo anapiga shutii lakini golikipa Manula anacheza vizuri, ilikuwa hatari langoni kwa Simba SC

90+2' Kuelekea kumalizika kwa mchezo

Almanusura Lusajo afunge bao, ilikuwa hatari sana lango la Simba Manula anacheza vizuri.. Lakini yupo chini akipatiwa matibabu

Kona kuelekea Simba, inapigwa kulee lakini Kanoute anaokoa.

Naaam mpira umekwishaaaaaa

FT: Simba SC 1-0 Namungo FC

....... Ghazwat...
Donoa hii
 
Simba tukimaliza runner up ni jambo lakushukuru aisee tuna mizigo mingi sana kwenye timu.hata champions league nawasi wasi tukaharibu records zetu zakufanya vizuri wacha tuone
Kwa sasa tumewekeza kwenye Ujenzi wa uwanja
 
Mtoto wa baba mdogo na Mtoto wa baba mkubwa walikuwa wanacheza leo!
 
Moses Scars Phiri ni mchezaji mwenye thamani kubwa sana kupitia miguu yake

Sijui kama wenzangu mnapata wasiwasi huu naoupata mimi kila muda napoangalia high performance ya huyu mwamba?

Hofu yangu ni kwamba misimu ijayo upo uwezekano wa kumkosa kwenye Club ya Simba na hiyo itachangiwa na kutojizuia kuonesha kiwango chake chenye high voltage kwenye michuano ya Club bingwa.

Hilo ndio eneo nalo hofia, huku ukanda wa Africa sina wasiwasi napo najua hakuna Club yeyote inayoweza ku afford bei yake, labda kama Simba iamue kumnunua tena
 
Back
Top Bottom