Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Agosti 17, 2022, ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, anakiwasha na Geita Gold kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.
Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90, kwa kila timu kuhitaji ushindi na hasa ukizingatia ndo mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili baada ya kufunguliwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023.
Kocha Zaron Maki wa Simba SC amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo wa kesho (leo) hakutakuwa mchezo rahisi, ni mechi ngumu dhidi ya timu ngumu, licha ya kupata muda mdogo wa kufanya maandalizi dhidi ya Geita, lakini anaamini atafanya vizuri.
Naye Kocha Msaidizi wa Geita Gold Mathias Wandiba amesema kuwa kwa upande wao wamejiandaa vizuri kwasababu wamepata muda wa kutosha kwa kujua wanacheza mechi ngumu dhidi Simba, kwahivyo wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi.
Nani kuibuka na ushindi wa mabao ya kutosha kwenye mtanange huu wa kwanza kwa timu zote mbili Ligi Kuu Tanzania Bara?
Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 12: 15 Usiku.. Usikose Ukapata Simulizi
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana