FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 3-0 Geita Gold | Uwanja wa Benjamin Mkapa | Agosti 17, 2022

FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 3-0 Geita Gold | Uwanja wa Benjamin Mkapa | Agosti 17, 2022

Leo tunaongoza ligi kwa mara ya kwanza baada ya kupita miezi mingi sana.
 
Kikos vip bado hawajatoa tu?? Mwenye nacho atupie bas
Kikosi cha Simba SC kinachoanza dhidi ya Geita Gold
20220817_173054~2.jpg
 
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Agosti 17, 2022, ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, anakiwasha na Geita Gold kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90, kwa kila timu kuhitaji ushindi na hasa ukizingatia ndo mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili baada ya kufunguliwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023.

Kocha Zaron Maki wa Simba SC amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo wa kesho (leo) hakutakuwa mchezo rahisi, ni mechi ngumu dhidi ya timu ngumu, licha ya kupata muda mdogo wa kufanya maandalizi dhidi ya Geita, lakini anaamini atafanya vizuri.

Naye Kocha Msaidizi wa Geita Gold Mathias Wandiba amesema kuwa kwa upande wao wamejiandaa vizuri kwasababu wamepata muda wa kutosha kwa kujua wanacheza mechi ngumu dhidi Simba, kwahivyo wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi.

Nani kuibuka na ushindi wa mabao ya kutosha kwenye mtanange huu wa kwanza kwa timu zote mbili Ligi Kuu Tanzania Bara?

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 12: 15 Usiku.. Usikose Ukapata Simulizi

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Leo Phiri kaanza,enhee semeni kabisa nani mwengine hajaanza.
 
Kwa kikosi hiki watani lazima mjipigie nyingi sana hawa wachimba kokoto, ila siamini iki kikosi amekipanga zoran hiki kitakuwa ni maelekezo tika bodinga ligi
 
Hapo kwa mtazamo wangu, Dejan Georgijevic angeanza, badala ya Banda.

Halafu sijajua hata Akpan hayupo kwenye benchi. Ngoja Tusubiri Kuona.
Huyo kocha ni bwege hamtaki Akpan
 
Back
Top Bottom