FT: Mashujaa FC 0-1 Simba SC | NBC Premier League | Lake Tanganyika Stadium | 03.02.2024

FT: Mashujaa FC 0-1 Simba SC | NBC Premier League | Lake Tanganyika Stadium | 03.02.2024

Hivi mechi nne za mwanzo ni za moto sana kwa kila mmoja. Tabora wakionesha ubora kama waliouonesha kwa Yanga. Itakuwa mechi ngumu sana kwa Simba
Siku ikifika usianze kuwalaumu tena Tabora kwamba wamecheza vibaya mkuu.
 
Hivi uwanja wa lake tanganyika umewekewa nyasi bandia? Na ule wa kagera sugar umewekewa nyasi bandia? uran
 
Usikariri mechi, angalia kinachotokea kwa wkt huu..
Hawa mashujaa wangepata utulivu wangeshapata bao....
Kusajili wachezaji wakubwa, kocha mkubwa, facilities nzuri tunategemea SIMBA ktk PITCH pawe na class na standard..

Si kwamba mashujaa wanacheza defence sana, ila ukiacha penalty, ni move ipi simba wamecheza ktk ushambuliaji..?
Achana na huyo Otorong'ong'o maana atakua ni either Mangungu au Try again na si vinginevyo.

Ila atakuja kuona tu kwamba timu yetu uongozi wake ni uchwara.
 
Hawa MASHUJAA Walirudishe hili jina kwa Wenyewe walikolitoa....!

Haiwezekani Wewe ni Shujaa halafu mtu atoke huko alikotoka , Akutwange hapo hapo Nyumbani Kwako..!

Nyumbani Lzm mtu Ukaze Kama alivyokaza Kagera mpaka Marefa Waingilie Kati ndo droo inapatikana...Eboo
Tulia.. watajirekebisha na kumtwanga Uto
 
Yeah! leo Tumekosa nafasi Tatu za Wazi.
Yule Fred mapema alikuwa anajaza.
Akaja Saidoo na Ubinafsi wake.
Akaja tena Fred, mahali pakushuti anatoa Assist kwa kifupi forward zilikuwa hazina utulivu.

kuanzia Dakika ya 59 mashambulizi yakahamia upande wetu, beki ikawa inacheza kama wanamabusha.
Kwa kifupi hawa Mashujaa wangekuwa na walau straiker/forward mmoja aggressive kidogo sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine hapa
Safari hii tunaweza tukashuhudia ligi tamu yenye ushindani wa timu tatu
 
Mkuu club bingwa cha msingi ni kufunga galaxy halafu draw na Asec ,lakini timu haina makali kabisa,heri pia tuwe na first eleven inayojulikana hata kama kuna rotation basi tunajua sub ikifanyika matokeo yanakuwa mazuri, ila tusubiri tu bado hayupo Inonga,Ngoma na Kibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Klabu bingwa, kama Asec akishinda na kisha Wydad akamfunga Galaxy basi safari ya Simba ya kwenda robo inaweza kuota mbawa
 
wydad alikaa 2 bila, aly ahly aliponea chupuchupu kwa kikosi hiki hiki kasoro ingizo kipya fred na jobe
Umeangalia upande huo, ila kikosi hiki hiki ndio kilichoshinda mechi moja tu ya kimataifa hadi sasa.
 
Klabu bingwa, kama Asec akishinda na kisha Wydad akamfunga Galaxy basi safari ya Simba ya kwenda robo inaweza kuota mbawa

Hata kama ikiwa Hivyo mechi ya Mwisho Galax atakutana Na Simba Dar es s salaam
 
Naomba kwa wanaoangalia Mpira,Simba wamebadilika au bado ni papatu papatu??

Saidoo Je,kabadilika au ni yaleyale?Natanguliza shukran.Maana hii timu yangu hainipi matumaini ya kutembea kifua mbele kabisa yani
Bado hatuna timu hapo
 
View attachment 2892593
All the Best Mnyama mkali.
Tukutane saa 10jioni kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)

Simba ya Dar es Salaam itashuka Dimbani, Uwanja wa Ziwa Tanganyika kuwavaa wenyeji wao Mashujaa FC.

Simba kwenye msimamo wa Ligi yuko nafasi ya 3. Amecheza michezo 10.
Akiwa na Alama 23. Anayeongoza ligi Azam FC ana michezo 13 na Alama 31.

Simba anaingia kwenye mchezo huu wa 11 akiwa na hasira baada ya kutoa suluhu na KMC mchezo wake wa ligi uliopita.

Mashujaa wao wako Nafasi ya 15 out of 16. wakiwa na alama 9 tu kwa michezo 12.

#nguvumoja#

Kikosi cha Mashujaa Kinachoanza.
View attachment 2892932

Kikosi cha Simba Kinachoanza
View attachment 2892924
Updates...

Lake Tanganyika imefurika,
Mashabiki ni wengi sana
Timu ndio zinaingia uwanjani.
Tuwe pamoja nitawajuza matukio yote muhimu kwenye hii game.
Tuwe sote,
Uran....

Dakika 0:40'
Mpira umeonekana kama hauna upepo ukabadilishwa

Dakika 4'
Mpira unaendelea inaonekana bado Simba hawajakaa vizuri.
Mpira uko upande wao sana.

Dakika 7'
Game on...
Mashujaa 0- 0 Simba.
Mpira umetulia bado hakuna mashambulizi makali kutoka pande zote.

Dakika 9'
Fred anakosa goli la wazi kabisa.
Baada yakutokea shambulizi kali kwenye lango la Mashujaa.

Dakika 13'
Simba wanapata penalti.
Ni penalty ya wazi kabisa.
Kibu D amefanyiwa madhambi ndani ya boxi la Mashujaa.
Ngoja tuone.

Dakika 16'
Goaaaaaaaaalllll
Simba wanapata goli la kuongoza kupitia mkwaju wa Penalti.
Anafunga Saidoo Ntibazonkiza.

Dakika 17'
Manula anaokoa shambulizi la mashujaa.
Game on...
Mashujaa 0-1 Simba

Dakika 24'
Game on...
Simba wanafanya mashambulizi yakushtukiza kwenye lango la Mashujaa.
Kanoute yuko chini mpira umesimama kidogo.
Anafanyiwa matibabu.

Dakika 27'
Mpira unaendelea.
Mashujaa 0-1 Simba

Dakika 29'
Simba wanapata kona, inapigwa inakuwa tasa.

Dakika 31'
Simba wanafanya shambulizi kali, Saido anapiga kick nyepesi sana inaishia kwenye mikono ya Kipa.

Dakika 37'
Kibu anaonekana kutumia akili zaidi kwenye lango la Mashujaa.
Free Kick.
Nje kidogo ya Mashujaa.
Saidoo anapiga inakuwa goal kick.

Dakika 39'
Mashujaa wanapata kona hapa.
Inapigwa haileti madhara.

Dakika 44'
Simba bado wanaumiliki mpira ila wanakosa mbinu za kufanya mashambulizi yenye impact.
Huyu Saido sijui kwa nini lazima acheze kila mechi .

Dakika 45'
Nyongeza ni 3'
Simba wanaendeleza kushambulia.

Half Time
Mashujaa 0-1 Simba....
===========================
Dakika 47'
Mashujaa wanapata free kick
wanaanza kwa short piece wanakosa maarifa wananyanganywa.

Dakika 52'
Mchezaji wa Mashujaa yuko chini, aligongana na Shabalala.
mpira umesimama kidogo.

Dakika 56'
Game On...
Mashujaa 0-1 Simba

Dakika 60'
Mashujaa wameonekana kufanya mashambulizi kadhaa kwenye goli la Simba.
Ila kukosekana kwa utulivu na maarifa mazuri hakuna madhara yoyote.

Dakika 61'
Simba wanapata kona,
inapigwa kona fupi ya haraka haraka pale ila inaishia kuwa goal kick

Dakika 65'
Kanoute anapata kadi ya njano.
Mashujaa wanapata free kick.
Inaunganishwa kwa kichwa inagonga mtambaa panya.
inatoka nje.
ni goli kick

Dakika 70'
Mashujaa wanafanya Sub mbili
Wanatoka wawili wanaingia Wawili.
Game On...

Dakika 71'
Chama Inn
Mzamiru Out

Dakika 74'
Inaonekana kuna mzozo kwenye benchi la ufundi la Simba na waamuzi, sijui wanalalamikia nini.

Dakika 77'
kuna mchezaji wa Mashujaa yuko chini pale,
Amenyanyuka Game on...

Dakika 81'
Kibu D out
Miquisonne Inn
Jobe Inn
Fred Out.

Dakika 85'
Game on..
Mashujaa wanafanya tena Sub mbili.

Dakika 89'
Benchika anaonekana kuhamasisha anapenda timu ishinde goli nyingi.

Dakika 90'
Nyongeza ni 3'
Ni dakika chache sana kulingana na muda uliopotea.

Dakika 90+2'
Saidoo Out
Kapombe Inn
Hamis Inn.

Full Time
Mashujaa 0-1 Simba

Huu ni ushida mwembamba kwa Simba.

#Nguvumoja#....
Saido kirusi
 
Saidoo anapambana sana.
Hao washambuliaji wapambane na sio kusubiri wapewe pasi na mpambanaji mwenzao.

Kibu D anapambana sana hadi kapata Penati iliyozaa goli.
 
Back
Top Bottom