FT: Mashujaa FC 0-1 Simba SC | NBC Premier League | Lake Tanganyika Stadium | 03.02.2024

Hivi mechi nne za mwanzo ni za moto sana kwa kila mmoja. Tabora wakionesha ubora kama waliouonesha kwa Yanga. Itakuwa mechi ngumu sana kwa Simba
Siku ikifika usianze kuwalaumu tena Tabora kwamba wamecheza vibaya mkuu.
 
Hivi uwanja wa lake tanganyika umewekewa nyasi bandia? Na ule wa kagera sugar umewekewa nyasi bandia? uran
 
Achana na huyo Otorong'ong'o maana atakua ni either Mangungu au Try again na si vinginevyo.

Ila atakuja kuona tu kwamba timu yetu uongozi wake ni uchwara.
 
Tulia.. watajirekebisha na kumtwanga Uto
 
Safari hii tunaweza tukashuhudia ligi tamu yenye ushindani wa timu tatu
 
Klabu bingwa, kama Asec akishinda na kisha Wydad akamfunga Galaxy basi safari ya Simba ya kwenda robo inaweza kuota mbawa
 
wydad alikaa 2 bila, aly ahly aliponea chupuchupu kwa kikosi hiki hiki kasoro ingizo kipya fred na jobe
Umeangalia upande huo, ila kikosi hiki hiki ndio kilichoshinda mechi moja tu ya kimataifa hadi sasa.
 
Klabu bingwa, kama Asec akishinda na kisha Wydad akamfunga Galaxy basi safari ya Simba ya kwenda robo inaweza kuota mbawa

Hata kama ikiwa Hivyo mechi ya Mwisho Galax atakutana Na Simba Dar es s salaam
 
Naomba kwa wanaoangalia Mpira,Simba wamebadilika au bado ni papatu papatu??

Saidoo Je,kabadilika au ni yaleyale?Natanguliza shukran.Maana hii timu yangu hainipi matumaini ya kutembea kifua mbele kabisa yani
Bado hatuna timu hapo
 
Saido kirusi
 
Saidoo anapambana sana.
Hao washambuliaji wapambane na sio kusubiri wapewe pasi na mpambanaji mwenzao.

Kibu D anapambana sana hadi kapata Penati iliyozaa goli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…