FT: MC Alger 2-0 Young Africans | CAF Championship League | December 7, 2024

FT: MC Alger 2-0 Young Africans | CAF Championship League | December 7, 2024

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Tyee!!! Leo nimewahi kuanzisha thread. Watakaonuna na wanune.
GeOQK9fWgAAtjk8.jpg

GeOT-tLWgAEiBAJ.jpg
Nastahili kupongezwa kwa mafanikio haya:

Mpira umeanza dakika 20 zilzopita. Ingawa MC Alger walianza kwa kasi sana
wakituhsmbulia kwa nguvu sana, tuliwadhibiti na hadi sasa bado tuko level ground ya NUNGE-NUNGE.

Pacome kapata Yellow card

Maadui wanatushambulia sana na wana miliki mpira kwa muda mwingi wao kwa wao lakini tunaendelea kuwadhibiti kabla hatifungua makombora yetu. Mpaka sasa dakika ya 33 hakuna madhara pande zote mbili


Tumeanza kuwawashia moto na naona kama maadui wanaishiwa pumzi kiodgo kidogo. Katika dakika hizi za mwishoni mwa kipindi cha kwanza maadudi wameanza kupagawa kwa hofu kuogopa nyundo linalopigwa na YASC


Sasa ni Half time, ila ineonekana kuwa AC Alger walikuwa nguvu ya Soda tu. Kama Kocha wa Yanga atajua kufanya Sub basi MC Alger watapigwa 0-2, ila kocha wetu akifanya makosa kwenye sub tutaishia ama 0-0 au tutafungwa 1-0 kwa bahati bahati.

Kipindi cha pili Kimeanza: Chama anachukua nafasi ya Azizi Ki. Mchezo umeanza kwa kasi ya kawaida kwa pande zote mbili. Hakuna matokea ya kutisha yalioyotokea katika dakika sita zilizopita tangu kipindi cha pili kianze.

Kuna kipindi waarabu walitaka kutunyanyasa mwanzoni mwa kipindi cha pili lakini tuliwadhibiti. Niwe mkweli Yanga hii inaonekana kuwa dhaifu sana kulinganishia na ile ya misimu iliyopita; sipendi kupata mshituko wa moyo tena.

Tumefungwa bao moja na Abdellahoiui dakiaka ya 64; sasa hivi tuko maji shingoni SUbstitutions za kocha huyu ni dhaifu sana. Alifanya papara ya substitution kabla ya kuona wapinzani watakujaje kipindi cha pili. Dube anatakiwa apewe muda wa kujitafakari kabla ya kupewa ulingo tena.

MC Alger wameleta Kipre Junior anayeijua Yanga vizuri sana


Kuna link hii hapa ya live stream


View: https://www.youtube.com/watch?v=y-68q2j_7ls

Zimebaki dakika chache tu mpira uishe na sioni matumaini ya ushindi tena kwani waarabu wamajizatiitit sana kwenye ulinzi sasa hivi.. Ni dakaika ya 87 sasa

Chama anapata kadi ya njano dakjika moja kabla ya mwisho wa dakika za majeruhi.


Tunadungwa bao la pili katika style ile ile tuliyofungwa na Al Hilal ya Sudan. Tumelaaniwa !! Sasa hivi tutabaki tunaiota robo fainali


Yanga ya sasa wana matatizo mawili makubwa: Ulinzi na ushambuliaji hafifu. Safu ya Ulinzi ni dhaifu, na safu ya ushambuliji pia ni dhaifu. Mzigo mkubwa kwa yanga ni aina ya mikataba waliyowapa wachezaji wao kwani sasa hivi wakiwafukuza watapata mzingo mzito wa kuwalipa bila faida yoyote. Bado ninapumua kwa haraka haraka sana ila siko kwenye drip. Kocha huyu hajui kuisoma timu ya wapinzani kabisa. Mambo mengi, muda mchache ngoja nitafute maji ya kunywa
 
Mimi ni Yanga damu, hii game tunafungwa Wachezaji wetu hawana morale kabisa, wamekata moto mapema. Kwa kifupi tunapoteza na hii.

Turudi na sababu kibao, ooh hali ya hewa oh mashabiki walitoa moshi n.k n.k
 
Back
Top Bottom