FT: Namungo 0-0 Yanga | VPL | Majaliwa Stadium

FT: Namungo 0-0 Yanga | VPL | Majaliwa Stadium

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Ligi kuu Tanzania bara inaendelea leo kwenye mchezo ambao Namungo ya Lindi inaikaribisha Yanga Sc kutoka viunga Jangwani na Twiga. Mchezo huu unachezwa katika uwanja wa Majaliwa ulio mkoani Lindi. Magoli yote ya pande mbili bado yamenuna.

=======

00' Mwamuzi apuliza kipenga kuashiria mwanzo wa mchezo

35'Saidoo yuko chini baada ya mchezaji wa Namungo kunyanyua mguu na kumgonga kwenye nyonga

37' Saidoo anchonga kona kuelekea lango la Namungo lakini haijazaa matunda

45+2' Mpira mapumziko

45' Mpira umerejea kutoka mapumziko

48' Namungo wanajaribu lakini Ibrahim Abdallah anakuwa upande wa kuotea wakati mpira unapigwa

50' Namungo wanapata kona lakini inakuwa mfu na kuzaa 'Counter'

52' Yacuba anajitahidi na kuingia ndani ya box lakini anapiga shuti kuuuubwa, Namungo 0-0 Yanga

55' Erick Kwizera anapiga kichwa maridadi akiunganisha mpira wa adhabu ndogo, mpira unapaa kidogo juu ya lango la Yanga

72' Shiza Kichuya anaingia kuchukua nafasi ya Hassan Manyanya

73' Yacuba anaweka kimiani kwa kichwa lakini kibendera anakataa

75' Fiston anaingia kuchukua nafasi ya Yacuba

90+3' Namungo wanagawana point na Yanga uwanja wa Majaliwa, Ruangwa. Namungo 0-0 Yanga
 
Wakuu mje kwenye huu uzi wa Yanga!. Yani hadi mashabiki wa Yanga mnaususa uzi wa mechi muhimu za Yanga kipindi hiki mwishoni mwa msimu wa ligi?
 
Wakuu mje kwenye huu uzi wa Yanga!.
Yani hadi mashabiki wa Yanga mnaususa uzi wa mechi muhimu za Yanga kipindi hiki mwishoni mwa msimu wa ligi?
Daaaa Uto wanakimbia Uzi
Ila wakisikia mechi za simba utawaona wanajazana na kucomment kwa wingi
Wamekimbia uwanjani sembuse huu uzi wao
Uto mko wapi? hii tabia ya kukimbia mliyoianza uwanja wa Taifa bado mnaendelea nayo mpaka huku kwenye uzi wenu?
Aiseeh kumbe wanafiki mumo wengi sana humu . Yanga ipo, na hata ninyi hampati usingizi bila kuchungulia Yanga wanafanya nini.
 
Fanyeni mtavyofanya lakini mjue lazima mcheze na Simba SC kabla msimu haujaisha, labda mhame nchi, kwasasa tuko SA tuna majukumu ya kuliwakilisha taifa.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Fanyeni mtavyofanya lakini mjue lazima mcheze na Simba SC kabla msimu haujaisha, labda mhame nchi, kwasasa tuko SA tuna majukumu ya kuliwakilisha taifa.
Hizi ndiyo akili za kimbumbumbu alikotaa Rage
 
Back
Top Bottom