FT: Namungo FC 1-3 Simba SC | VPL | Majaliwa Stadium

FT: Namungo FC 1-3 Simba SC | VPL | Majaliwa Stadium

Wahi ziko chache
FB_IMG_16217694080943737.jpg
 

Attachments

  • IMG-20210529-WA0050.jpg
    IMG-20210529-WA0050.jpg
    96.2 KB · Views: 1
Pamoja na hayo bado kwangu Mimi mugalu siyo striker mzuli. Kabla ya goli na assist hakucheza vizuri.
Ukitaka kujua ubovu wa mugalu usiwe na mihemko, angalia movement zake na jinsi anavyoji position wakati tunashambulia na utofauti na bocco anachofanya wakati tunashambulia.
Goli alilofunga ndiyo position anazotakiwa kukaa mshambuliaji wakati wa kushambulia lakini Mara nyingi huwa hakai vile.
Kabla ya goli kampa mipira mingapi kagere kablow?
 
Ila jamani hali ya viwanja lazima lifanyiwe kazi msimu ujao
Sijui watakuja kuyafanyia kazi lini.
Mimi ningekuwa na mamlaka Viwanja vya michezo ni first priority kwakweli. Serikali haijui kuwa viwanja ni sehemu mojawapo kubwa ambayo unaweza kuuza sura ya nchi.
Anza na
CCM Kirumba, Jamhuri zote, Arusha, Shinyanga, Sokoine na vingine.
 
Dah ila mkuu nilikuwa natoka jasho acha tu nilikuwa nimebana usinga kwapani saivi kwapa linauma[emoji23]

Mimi je? Nilikuwa nakunywa Nederburg Barone haipandi,najifanya kufuatilia H/work za watoto,mara narukia topic ya kina Magige huko,huku narefresh hii page kuona kinachoendelea. Mweeh Ushabiki huu utakuja tupeleka pabaya haki[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pongezi kwa benchi la ufundi la Simba kwa kumuingiza Dilunga maana hapo ndio meza ilipopinduka. Simba walikosa mtu wa kuifungua Namungo kutokea kwenye nusu ya tatu ya uwanja kumbe Dilunga ndiye aliyekuwa na funguo hiyo ya ubunifu. Na hapo ndio umuhimu wa kikosi kipana unapoonekana. Simba walikuwa taratibu sana kipindi cha kwanza kiasi timu ilikuwa haiendi mbele kwa kasi ukiacha "long pass" za Wawa lakini muda wote wa dakika 45 za mwanzo benchi la ufundi hawakuliona hilo tatizo. Lakini mabadiliko ya wachezaji kipindi cha pili ndio killichowasaidia kupata matokeo. Pia Simba wawe makini sana wanapocheza mechi zao kwenye viwanja vya mikoani wasiwe wanajaribu kucheza "pira biriani" kwani viwanja vingi mikoani sio rafiki sana na iana yao ya mchezo na hii ilionekana wazi kwenye kipindi cha kwanza. Simba wanatakiwa wakifika mikoani wajitahidi kutafutra matokeo zaidi hii habari ya "pira biriani"wasubiri wakirudi kwa Mkapa au kwenye viwanja vizuri kama Kaitaba. Vinginevyo ipo siku watalizwa na hawataamini matokeo.

Bahati mbaya sana kwa Namungo walibaki sana nyuma na walishindwa kuimaliza mechi mapema kwa "counter attack". Kwa hiyo Namungo wanapaswa wajilaumu wenyewe kwani wakati wanaongoza goli moja ilifika mahali kipa wao anapoteza muda badala watafute goli la pili wakati mpira ulikuwa bado dakika nyingi sana. Kocha wa Namungo ni kocha mzoefu alishindwa nini kuwajulisha wachezaji wake waache kupoteza muda kwa kigezo cha kuongoza goli moja wakati inajulikana kabisa duniani kote unapochezawa mpira kuwa goli moja huwa linarudi hata sekunde ya mwisho?

Poleni sana Namungo na hongereni Simba.
 
Back
Top Bottom