Nimependa tu wachezaji walivyokuwa wanampa ushirikiano Saido.
Ile header ya Kibu baada ya kuzuiliwa mpira ukatua karibu na miguu yake halafu nyavu hizi hapa.
Alichokifanya ni kumzuia beki asije kuutoa mpira na kumpisha Saido apachike goli.
Bocco naye nilimuona mara nyingi akiwa anafanya hivyo sometimes alikuwa yuko mbele ya box halafu Saido yupo nyuma.
Bocco alikuwa ana hold mpira kumfanya Saidi asogee ili ampe pasi aweze kufunga.
Hii ni bonge ya team work na leo angekuwepo Chama mpishi wa assist, Saido angetoka na goli 8 watu wangesema Simba imenunua mechi.