FT: Niger 0-1 Tanzania. Kufuzu Kombe la Dunia. Novemba 18, 2023

FT: Niger 0-1 Tanzania. Kufuzu Kombe la Dunia. Novemba 18, 2023

Kwenye kundi letu wangejituma kidogo tu,ukiachana na Morocco,wengine wote ni wa kawaida sana. Kwa sasa sisi tunaweza kuwa level moja na Zambia.

Nimeangalia mechi ya DRC na Zambia. Hawa DRC wepesi mno. Hapo za kuwekana sawa inatakiwa iwe Zambia na Moroco tu. Wachezaji wakikaza kidogo tu hawa Niger ni wetu hawa,inatakiwa tuwatupie nje,ndani. DRC pia kwa walivyo sasa tuwatupie nje,ndani. Hapo inatakiwa wakija Moroco tupige nao patulo sale. Kwao acha watufunge. Tupambane na Zambia kwao sare,hata kwetu tukipata nao sare.

Hapo tayari tutakuwa tumemaliza na point 11[emoji3581] . Tutakuwa tumepita nafasi ya pili. Hata tukiangukia nafasi ya 3,kwa kundi letu ksbb ziko 5 maana yake timu ya 3 kuna timu itacheza nayo best rooser mtoano ndani na nje.

Kizuri zaidi timu sasa kutoka Afrika zimeongezwa nafikiri zitakuwa kati ya timu 9 au 10 hapo. Kwa hiyo sidhani kama tutakosa. Kocha kama mjanja waangalie sana mechi za DRC na Zambia,maana huko kuna point zetu wachezaji wakiongeza moto kidogo tu
Sio DRC wewe.

Ni Congo Republic ile ya Brazzaville
 
Wanajitahidi halafu bado wadogo hata maturity yao unaiona kama tukiendelea hivi miaka kama mitano tutafikia level ya kutambulika Afrika
Maturity tena?
Mbona wengi hapo umri umeenda?
 
Match haijapewa uzito stahiki.., kila mahali watu wamekomaa na mabango ya Yanga, nimeshajua nini kinadumaza mpira wa bongo. Ni simba na Yanga. Maana wanapika wachezaji wa kigeni wanaoenda kuzipaisha nchi zao, huku sisi tukidumaa
Vilabu vina malengo yao, Tff ndio wenye jukumu la kuandaa vijana kujenga timu ya taifa, vilabu ni wadau tu.
 
Maturity tena?
Mbona wengi hapo umri umeenda?
Kun madogo wengi sana Bacca,Job,Novatus, huyo aliye funga goli, wapo wengi sana yaani kuna kitu una kiona cha msingi tusimame kwenye project na mipango yetu.Ila progress naiona.
 
Kun madogo wengi sana Bacca,Job,Novatus, huyo aliye funga goli, wapo wengi sana yaani kuna kitu una kiona cha msingi tusimame kwenye project na mipango yetu.Ila progress naiona.
Mpango bila Uzalendo hakuna
 
Hata comment yako siyo ya kizalendo kabisa....ni comment ya hovyo na iliyojaa shutuma dhidi ya vijana wetu wanaolipambania taifa ukiwemo wewe ndani yake...huna haki kabisa kusema au kuandika kuwa eti vijana wetu hawaonyeshi uzalendo...
Umesema kweli. Wengi wetu tunachojuwa ni lawama. Kukosea katika mchezo ni kawaida lakini sisi huku nje tumejikita katika kutafuta makosa (mabaya) ya timu. Kama unauangalia mpira na nia ya kutafuta makosa, lazima utayapata. Let us be positiove. Hata mtoto wako kama kila siku ni matusi ya kumkatisha tamaa unafikiri atafanya vizuri!
 
Back
Top Bottom