FT: Niger 0-1 Tanzania. Kufuzu Kombe la Dunia. Novemba 18, 2023

Taifa stars hawatii moyo kabisa kuwatazama, hapa usilaumu watu wakulaumiwa ni tff kushindwa kua na mipango ya kueleweka. mwisho wake timu imepoteza mvuto.
 
Ukuta wa Berlin wa Yanga umeonesha kiwango Cha juu Manula Yuko likizo Leo zile 5G kumbe ni beki mbovu

Timu ilikosa muunganiko wa katikati na mbele, viungo Wote watatu Fei, Mnoga na Bajana walikaba zaidi na kusahau kupandisha timu.

Timu iliishiwa pumzi dakika 20 za mwisho ikawa roho mkononi hivyo wafanye mazoezi sana ya mbio na fitness gym , Morocco sio Niger wasijetuaibisha 5G kwa Mkapa!

Ila timu yetu imekaba vizuri, ila nawapongeza sana Mbwana Samata na Simon Msuva kwa kujituma sana kukaba mwanzo mwisho kuliko wachezaji wengine , big up sana mmeonesha mfano wa kuigwa.

Manula na Mwamnyeto Kuna mpira walitegeana jamaa wa Niger akawa anaenda kufunga ila Nondo akawahi kuokoa Boko lake Hili wasirudie, waongee!!

Novatus ni majeruhi wamtibu haraka Leo alihangaika na msuli wa paja mara kwa mara kacheza kwa uzoefu tu Kuna saa alichuchumaa ikawa anacheki kama anaweza kuendelea.

Samatta alikuwa wa moto sana ila viungo hawakumlisha mipira vizuri Mudathir acheze next match japo kipindi kimoja.

Morocco tuwachezee kama jinsi tulicheza na Algeria timu nzima ikabe kwa nguvu kwa dakika 90 hatufungwi.

Otherwise hongera sana Taifa Stars jezi ya njano na blue inatubeba sana!
 
Huna akili mkuu
 
Kwa jinsi alivyopokea Ile pasi na ku dribble nikajua huyu hachezi soka Tanzania
Maji na mafuta hujitenga, mchezaji wa kibongo utamjua na wa mbele utamjua tu.

Kuna faida kubwa ya wachezaji kucheza nje ya nchi. Viwanja vyetu vingi vya ndani, nature ya wapinzani NBC pira papatu papatu kwa kiasi fulani halikwepeki.
 
tatizo huwa linaanza hapa mnaleta siasi kwenye mambo yanayotaka sayansi nasio porojo.
Kama ni siasa michezoni zimeletwa na hao hao waliopo madarakani, mambo ya sayansi michezoni yanahitaji kizazi kingine na sio kizazi hiki cha kununua magoli.
 
Leo Yanga imecheza na Niger...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…