FT: Niger 0-1 Tanzania. Kufuzu Kombe la Dunia. Novemba 18, 2023

Wewe hizi taarifa za best loser umezitolea wapi? Africa tunapeleka timu 6 tu na makundi yapo 6 tu.
Kweli? Mbona walisema zimeongezwa timu? Au yale ya mbele?. Ngoja nifuatilie tena,huenda nimechanganya na kombe la dunia la mbele
 
Wewe hizi taarifa za best loser umezitolea wapi? Africa tunapeleka timu 6 tu na makundi yapo 6 tu.
Hivi hapa umeandika kutokana na kutojua au unabishana? Kwa nini kabla hujaonyesha u... Usingeenda hata LiveScore au google ukajiridhisha na ulichotaka kuandika? Kukusaidia tu, jumatatu (20/11/2023) kutakuwa na mechi za group I, sasa rejea herufi I ni ya ngapi kutoka herufi A.
 
Kwa mpira waliocheza stars ni matumaini hakuna.
Bado inaonekana tuna shida ya kocha
 
Jana nmeona timu ya taifa mpya kabisa, ile iliyocheza na Algeria imeenda wapi?

maana wamecheza hovyooo mnooo hawakutahli kupewa ndege kabisa

Ile kama ndyo tim ya taifa kunahaja ya kufanya review

au watatuletea tim nyingne itakayo cheza na Morocco?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatuna Wachezaji hasa kule mbele.Samata hamna kitu Huo ndio ukweli.
Kubali tu mkuu kuwa kocha ni tatizo stars. Hata huyo Samata mbovu anapangwa na kocha.
Kocha ndie anaamua timu ichezeje
 
Hatuna Wachezaji hasa kule mbele.Samata hamna kitu Huo ndio ukweli.

Mkuu mechi ya jana timu ilikua haijengi mashambulizi
Mipira karibu yote ilikua inaishia katikati ya uwanja
Sasa hao akina mbwana mipira itawafikiaje?

Mfumo ulikua kujilinda zaidi na mashambulizi ya kushtukiza lakini penetration pasi zote zilikua fyongo

Hata hivyo tushukuru plan ya mwalimu ililipa tulipata nafasi tukaitumia na tukalinda vizuri sana
 
Kubali tu mkuu kuwa kocha ni tatizo stars. Hata huyo Samata mbovu anapangwa na kocha.
Kocha ndie anaamua timu ichezeje
Kuna jamaa anasema plan ya Mwalimu ilikuwa kujilinda!
 
Samatta na Manonga walikosa magoli ya wazi kabisa.Samattta alibaki na kipa na Manonga alibaki na goli bila kipa wakakosa!
 
Umeonekana kabisa wewe ni yanga
 
Mbona fei ndiyo kaongoza kupiga pass za macho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…