FT: Nyasa Big Bullets 0-2 Simba | CAF Champions League (CAFCL) | Bingu Stadium

FT: Nyasa Big Bullets 0-2 Simba | CAF Champions League (CAFCL) | Bingu Stadium

Nusu fainali ya CAF kwa kiungo cha Mzamiru na winga Kibu ni ndoto za mchana.
 
Israel!......njia hii. Toka mechi ya mwisho Sudan alikimbizwa na yule Mkongo sikuwa na imani nae.

Hakuna beki wengine? Matola anamuamini nini huyu dogo? Ndio maana wengine wanasuspect kuwa anachukua 10%
Kapama anakanyaga beki mbili vizuri tu,hata Nyoni akiwa Azam alikua anacheza half back 2.mzee Onyango akiwa Arambee star ana wekwa mbavu ya kulia na anakiwasha mpaka nyasi zinang'oka.
 
Mchezo umeanza

Timu zimeshaingia uwanjani kuelekea kuanza kwa mchezo huu

Kikosi cha Nyasa Big Bullets

Kikosi cha Simba kuelekea mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets, leo Jumamosi Septemba 10, 2022, unatarajiwa kuanza saa 10:00 Jioni kwa Tanzania.


Klabu ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wapo ugenini wakitarajia kushuka katika Dimba la Bingu National Stadium nchini Malawi kukinukisha dhidi ya wenyeji Nyasa Big Bullets katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo unategemewa kuwa wa ushindani ndani ya dimba ambapo Nyasa Big Bullets ni timu ambayo ina wachezaji wenye uwezo kuuchezea mpira miguuni hivyo si timu rahisi, hivyo unatakiwa uwe umejiandaa vilivyo kuchuana nao.

Hivyo basi tunatarajia kuona burudani ya kukonga nyoyo, ambapo Simba SC wakiwa na wachezaji wao mahiri wenye vipaji na experience kubwa kwenye michuano mbalimbali ya CAF watakavyoingia na mbinu ngumu ya kuhakikisha wenyeji wanakuwa na wakati mgumu muda wote wa mchezo.

Kwa yote haya ni ndani ya kuamua...Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:00 Alasiri..Usikose Ukapata Simulizi..Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

Karibu Jopo Zima la Lunyasi Mwifwa, OKW BOBAN SUNZU, Scars, Kinyungu, denooJ, Kalpana, Shunie, Mshana Jr, BRN, Mawawa, mpiga vichwa, koboG, Waminyato, Pettymagambo, SAGAI GALGANO, Troisième Ceil, 3ZOV, Proved, mkwepu jr, Satoh Hirosh, Elli, MTAZAMO, Designer_3434, TUJITEGEMEE, Mac Alpho, Kiweriweri, Donnie Charlie, CHIEF PRIEST, rodrick alexander, Chaliifrancisco, Mtoto halali na hela. Na wengine wana Lunyasi [emoji881][emoji881][emoji881] Nguvu Moja

===========

Vikosi vyote vya Nyasa Big Bullets na Simba SC vimefika katika Dimba la Bingu National Stadium [emoji2522] tayari kwa mchezo.
Nyasa Big Bullets ushindi lazima
 
Big Bullet kule tukimpiga kama goli mbili hivi au zaidi hapo sasa huku Lupaso Ntwala tunamalizia tu kwa vinywaji laini kama juis,maji baridi na Al qasus mujarabu.
Hii mentality ya kuingia uwanjani tukiamini tayari tumeimaliza mechi ndo ambayo huwa inatucost sana, nikikumbuka ya UD SONG, JWANENG na KMC juzi nabaki kusikitika tu.

Inatakiwa game zote tunakaza kama hatujapata kitu.
 
Back
Top Bottom