mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,126
- 5,068
Leo tarehe 10 April 2022 majira ya saa 16:00, Mnyama hatali Sana , mnyama mwenye njaa ,, mfalme wa nyika , Club ya 12 kwa ubora Africa nzima,, club ya 12 miongoni mwa vilabu vya soka Africa nzima, simba sports club atakuwa na mazoezi ya kupasha misuri pale atapofika kumfundisha mazoezi ya viungo mpaniaji wa mechi hiyo Police Tanzania FC huko mjini Moshi Kilimanjaro!!
Sina mengi , karibu tujumuike masaa machache yajayo tuone mnyama anavyopasha msuri !
Kila la kheri Mnyama Simba!!
Kijan na njano wanaweka record Leo ya kufurushwa kwenye michuano ya shirikisho na kijitimu aka GGM
Utopolo mpambane na hali yenu
=========================================
LIGI KUU: SIMBA YAAMBULIA POINTI MOJA KWA POLISI TANZANIA
Simba imeambulia pointi moja katika mchezo wa ugenini wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania kwa matokeo kuwa 0-0 kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi, leo Aprili 10, 2022.
Simba imefikisha pointi 41 na kujitengenezea mazingira magumu ya kutetea ubingwa wake kwa kuwa Yanga ipo kileleni ikiwa na pointi 51, hivyo kuna tofauti ya pointi 10, timu zote zikiwa na michezo 19. Polisi wapo nafasi ya nane wakiwa na pointi 24.
Baada ya mchezo huo Kocha wa Simba, Pablo Franco alisema ni ngumu kucheza mechi mbili ndani ya siku mbili, alifanya mabadiliko ya kikosi ili kukwepa wachezaji kuumia kuelekea mchezo ujao kutokana na hali ya uwanja kutokuwa nzuri