Mechi ya ufunguzi wa Kundi K kwenye Kombe la Dunia 2026 kati ya Portugal na DR Congo imekwisha kwa sare ya 1–1, mchezo ukiwa na mvuto mkubwa kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Portugal walitangulia kupata bao la mapema dakika ya 6 kupitia João Neves kwa kichwa safi baada ya krosi nzuri, wakionekana kuanza kwa nguvu na kumiliki zaidi mchezo.
Hata hivyo, DR Congo hawakukata tamaa. Walipata bao la kusawazisha dakika za mwisho za kipindi cha kwanza kupitia Yoane Wissa (dakika 45+), akiunganisha krosi ya kona na kuamsha shangwe kubwa uwanjani.
Baada ya hapo, mchezo uliendelea kwa kasi lakini mabeki wa pande zote mbili walisimama imara, na matokeo yakabaki 1–1 hadi kipenga cha mwisho.
================
Wa Afrika wengine wapo uwanjani leo tena DR Congo saa mbili usiku unaweza kusema wakina Mayele.
Watafanya nini mbele ya wababe Ureno wanaongozwa na CR7?
Moja ya Takwimu za moto kwa timu zote
Ureno
Ureno wanaingia kwenye Kombe la Dunia kama miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, na hiyo haishangazi ikizingatiwa kwamba wamepoteza mechi moja tu kati ya 13 zilizopita (Wakisbiri 10, Sare 2). Isitoshe, mchezo wao wa mwisho wa kiushindani uliisha kwa ushindi mnene wa mabao 9-1 dhidi ya Armenia kwenye mechi za kufuzu!
Hata hivyo, kuhamishia kiwango cha namna hiyo kwenye jukwaa la Kombe la Dunia imekuwa changamoto ya muda mrefu kwa Ureno, ambao wamefika hatua ya nusu fainali mara moja tu tangu mwaka 1966! Kuanza vibaya kumekuwa kukiwaangusha katika michuano ya hivi karibuni; wameshinda mechi moja tu kati ya nne zilizopita za ufunguzi wa Kombe la Dunia (Sare 2, Kupoteza
1).
Mechi tatu zilizopita kati ya hizo zilizalisha jumla ya mabao 15, ambapo mabao matano yalipatikana kwenye ushindi wao pekee dhidi ya timu nyingine ya Afrika, Ghana, mnamo 2022 (3-2).
DR Congo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo)
DR Congo wanarejea kwenye jukwaa la Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974, ambapo kipindi hicho walishiriki kama Zaire na kupoteza mechi zote tatu bila kufunga goli lolote, huku wakiruhusu jumla ya mabao 14! Kusubiri kwao kumeshika nafasi ya nne kwa kuwa kwa muda mrefu zaidi kati ya fainali mbili mfululizo, na kusubiri huko kulihitimishwa kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamaica kwenye mechi ya mchujo ya mashirikisho (inter-confederation play-off) mnamo mwezi Machi.
- Ureno: Walikuwa wamefunga goli katika mechi 10 mfululizo za Kombe la Dunia kabla ya kufungwa na Morocco kwenye hatua ya robo fainali mwaka 2022.
- Mabao ya Ureno: Mechi 9 kati ya 13 zilizopita za Ureno zilimalizika kwa kufungwa jumla ya mabao 3 au zaidi (over 2.5 goals).
- DR Congo (Ushindi): Katika ushindi 22 uliopita wa DR Congo, ushindi wa mechi 18 ulipatikana bila wao kuruhusu goli hata moja (clean sheet).
- DR Congo (Magoli ya kufungwa): Kila goli kati ya manne yaliyopita ambayo DR Congo walifungwa, lilifungwa baada ya dakika ya 50 ya mchezo.
Updates
Mapema tu Neves anaweka chuma ya moto Ureno 1 DR Congo 0