Nadhani hii ni mara ya kwanza final kufanyika game moja tu neutral ground sasa hili ni shida sio utamaduni wetu sababu ziko nyingi. Mpira wa Africa unategemea na viwanja vya nyumbani washabiki kutengeneza shamrashamra na figisu nyingi ndio zinafanya final kunoga ukipeleka neutral ground washabiki wa team hizi kusafiri kwa hali zetu Africa umaskini gharama kubwa na visa sio rafiki sasa wenzetu ulaya kwanza visa free halafu kiuchumi wako vizuri na usafiri ni rahisi ndio maana final zao hazijalishi zinachezwa wapi zinakuwa full na hamasa. Nadhani turudi katika mfumo wetu wa home and away, na viwanja Africa sio vizuri haya tuje kufanya siku Africa nzima visa ziwe free na usafiri uwe wa uhakika. Ni sawa Simba na Yanga waingie final halafu uwapangia final Libya unategemea nini?