FT: Simba 0-1 Al Ahly | CAF CL Robo Fainali | Benjamin Mkapa Stadium | 29/03/2024

FT: Simba 0-1 Al Ahly | CAF CL Robo Fainali | Benjamin Mkapa Stadium | 29/03/2024

Ki ukweli sijaumia....sijui kiroho hii imekaaje...
Samaleko
20240229_140725.jpg
 
Sina mengi leo,
Sina solidarity kwenye mambo ya kipumbavu.
Naomba makolo mniambie Shomary kapombe ana tatizo gani..?
Hana confidence, hana speed, anafanya makosa mengi sana binafsi. Shida ipo wapi..?
 
Nichukue wakati huu kuwakaribisha kesho kwenye burudani tukufu muda ndo ule ule waliofir*wa watu leo.
Simu ziite
 
Timu imecheza vizur bahati tu imekosekana, ila Hawa waarabu Wana ujinga mwingi sana jamaa kabebwa kwa machela ka relax akijidai anaugulia maumivu kafika nje ya uwanja karuka fasta anataka kuingia tena uwanjani
Ikiwa upande wenu mnaongoza ni furaha sana kupoteza muda ila ikiwa tofauti huwa ni maumivu makali. Hata simba ingepata nafasi ya kuongoza ingefanya hivyo.
 
Timu ya kufika semi final hatuna, Kuna kitu mgt au mashabiki hawajakubaliana nacho, timu ni project kama project nyingine tu, katika timu zilizokuwa na kikosi kizuri misimu kadhaa nyuma ni Simba, ni kama mgt haitaki kujua au haijui kuwa inaipeleka timu wapi, nusu fainali ya mdomoni tu!. Kwanini huoni future kwenye hii timu?, kwasababu hiyo future haipo kwenye timu hii, lazima maamuzi magumu yafanyike ya kuwa na mgt ya mpira na kuacha baadhi ya wachezaji wetu pendwa lazima tukubali ukweli huu.

Kama utakuwa unaangalia mpira vizuri unaona kabisa Simba inarudi ilipotoka, hata succession plan inaonekana timu Haina na timu tayari ishapoteza ile "Culture" yake. Tatizo ninaloliona Bado Simba Haina mgt ya mpira, Bado ina akili zile za kizamani za mpira furaha.

Fikiria tu Hadi Sasa una mchezaji tegemeo kama Saido, Chama, Kapombe, Tshabalala and where is our football heritage? nk hivi serious kweli?, unataka uende semi final na unawategemea Hawa kweli?, una lundo la wachezaji wengi wanaotakiwa kuondoka maana hawana tena cha kuoffer kwenye timu. Timu zote zinazojitambua duniani huwa na succession plan za wachezaji, Kila msimu lazima mgt ijue nani wa kuondoka nani wa kubaki.

Hakuna cha kujipa moyo sijui Kuna mchezo wa pili sijui Nini, hayo ni maneno ya mtu asiyejitambua Kila siku wewe hupigi hatua maana yake unakosea Kila siku, binafsi nawapongeza YANGA SC sana Kwa project Yao kama wakiendelea hivi wanamuacha SIMBA, project ya mpira ni endelevu inayotakiwa kuendelea mbele Kwa kuonesha matokeo siyo hii ya Simba.

Hii unachokionyesha hapa kinaitwa ' ngozi nyepesi'

Hii mambo Waachie Wenye ngozi ngumu
 
Back
Top Bottom