Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 16,908
- 19,123
Kabisa...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabisa...
Naam nakukubalia kabisa Simba leo awakua sawa japo ushindi umepatikana.Lengo limetimia ila Mgunda kuna kazi unatakiwa kuifanya. Timu leo haikucheza vizuri.
kishindo kiko wap, namungo alimpiga nyingi sana huyoHatareeeeeeeew
Fulll timeeeee
Makundi kwa kishindoooo
4 VS 1
Lingekuwa kosa kubwa sana kujichosha wkt tulishafuzuLengo limetimia ila Mgunda kuna kazi unatakiwa kuifanya. Timu leo haikucheza vizuri.
Tusibiri kishindo chako cha kutolewa kitakuwaje. Inaonekana hiki cha Agosto hakijakuridhishakishindo kiko wap, namungo alimpiga nyingi sana huyo
jana mamelod katimba kwa goli 15 wewe nne unaita kishindo kweli kolo n kolowizad
Ni siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu sana na mashabiki hapa Tanzania, kule Angola na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Mnyama mkali anashuka dimbani akiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao matatu kwa moja ugenini.
Anaenda kumaliza ngwe na kuingia hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa wa Afrika.
Tutakuwa hapa tukipeana taarifa mubashara. Mechi itaanza saa kumi kamili Alasiri.
Kikosi cha mnyama mkali
=======
01' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo dimba la Benjamin Mkapa.
03' Moses Phiri anafika lango la De Agosto lakini anadondoka mwenyewe.
07' Simba wanacheza pasi fupi nyingi ndani ya nusu yake.
12' Simba wapata kona ya kwanza ya mchezo, kichwa cha Inonga kinapaa juu ya goli.
13' 🟡Many Rashid wa De Agosto analamba kadi ya kwanza ya njano baada ya kumdondosha Okra akielekea langoni.
20' Mpira uko chini zikiwa ni pasi maridadi kutoka kwa timu zote mbili.
21' Simba wanapata kona ya pili ambayo inashindwa kuleta mabadiliko kwenye ubao.
25' Sakho anapunguza watu na kuingia mwenyewe, beki wa De Agusto anapangua mipango.
30' Phiri na Okrah wanajaribu langoni mwa De Agusto, gonga yao inazaa kona ya tatu kwa Simba bila ya matokeo.
32' 🟡 Kadi ya njano kwa Venancio baada ya kumvuta shati Chama.
33' [emoji460]Moses Phiri anaiandikia Simba bao la kwanza, pasi safi kutoka kwa Zimbwe Junior aliepokea mpira kutoka katikati ya uwanja.
43' Onyango anauza mpira, free kick kuelekea Simba. Free kick ya De Agosto inagonga ukuta.
45+2' Mpira mapumziko.
=====
50' Okra anajaribu kuwapita walinzi wa De Agosto lakini anapiga njeeeeee.
51' Venancio anapewa onyo kali baada ya kumzuia Kanoute kwenye njia, Venancio tayari ana kadi ya njano.
58' Simba wanamiliki mpira kwa kiasi kikubwa katikati ya dimba huku wakijaribu kufika kwenye lango la De Agosto mara chahce.
59' Faulo ya tisa kwa De Agosto, Mzamiru yuko chini.
63' Simba inapoteza mpira baada ya kujaribu kona fupi, mpira wa kurusha kuelekea Simba.
64' Chama anafanya udambwi na kumpita mlinda Mlango wa De Agosto, pasi inashindwa kimfikia Moses Phiri.
65' Phiri anapata nafasi nyingine na kuachia mkwaju mkali, kipa anapangua. Kona.
68' [emoji680] Kibu Deniss anaingia kuchukua nafasi ya Sakho.
72' 🟡 Antonia Silva anapewa kadi ya njano kwa kumchezea ndivyo sivyo Okra.
77' [emoji680]Habib Kyombo anaingia kuchukua nafasi ya Okrah aliyeumia.
78' [emoji680] Zimbwe JR nae anaenda bench na nafasi yake inachukuliwa na Gadiel Michael Mbaga.
87' Gadiel anapewa kadi ya njano baada ya kuvuta bukta ya mchezaji De Agusto.
89' Manula anaingia mwenyewe mpaka katikati ya uwanja.
90' Dakika tatu zinaongezwa kuhitimisha mpambano.
90+1' Nyoni na Mkude wanaingia, Israel Mwenda anaenda bench.
90+3' Mpira unatamatika dimba la Benjamin Mkapa na Simba wanasonga mbele kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa jumla ya mabao 4-1 dhidi ya De Agosto.
Kila msimu ni maneno hayo timu zinakataa kupangwa na Simba group moja halafu hao hao wanabeba makombe wakati Simba akiwa na furaha za kuongoza kundiHaya Sasa, Kuna Timu zimeanza Maombi KAFU kutokupangwa Na Simba Group Moja
1. Al Ahaly- Egypt wanakataa kabisa kupangwa na Simba
2. Al Hilali Sudani- Wamesema Wakifuzu Leo Wasipangwe na Simba Group Moja
3. Esperence Ya Tunisia Wakataaaa kabisa Kupangwa Na Simba
na mamaako anasemaje ?Haya Sasa, Kuna Timu zimeanza Maombi KAFU kutokupangwa Na Simba Group Moja
1. Al Ahaly- Egypt wanakataa kabisa kupangwa na Simba
2. Al Hilali Sudani- Wamesema Wakifuzu Leo Wasipangwe na Simba Group Moja
3. Esperence Ya Tunisia Wakataaaa kabisa Kupangwa Na Simba
Nawaombea mfuzu piaKila msimu ni maneno hayo timu zinakataa kupangwa na Simba group moja halafu hao hao wanabeba makombe wakati Simba akiwa na furaha za kuongoza kundi
Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
nini cha ajabu??Kwa mara ya kwanza Kocha MTz kaipeleka timu makundi CAFCL bila kupoteza mchezo Wala droo
Ww acha kupambana na Simba ww utakufa kibudu. Hiii ndo Simbaa 4 kwa 1 hutaki nenda kacheze ww au wpe timu yako mbovu ya Utopwizo wapigwe ndani nje. Simba ya sasa haina Away wala Home kote tunapigaaa. Sisi hatuna haja na historia kwa sbb Agosto ya juzi sio ya leo,man up brookishindo kiko wap, namungo alimpiga nyingi sana huyo
jana mamelod katimba kwa goli 15 wewe nne unaita kishindo kweli kolo n kolowizad