Nyie viande ile ni derby, Derby ina mambo mengi, unaweza ukawa na wachezaji wazuri na ukapoteza mechi au ukashindwa kupata matokeo
Katika kile kipindi ambacho Yanga ilikuwa mbovu sana, mlitufunga goli moja kwa Morrison
Wakati huo ukumbuke sisi tuna kikosi bora na kipana kuliko nyinyi.
Tukaja kwenye mzunguko wa pili tukawapiga goli mbili kipindi cha kwanza, kipindi cha pili mkarudisha zote na mechi kuisha ikiwa ni sare.
Hizo zote ni mechi za msimu mmoja na kikosi kimoja huku nyinyi mkiwa na kikosi kibovu lakini bado hatukuweza kuwafunga.
Kuwa na kikosi kizuri au wachezaji bora bado kwenye ishu ya Derby sio kitu cha kutegemea sana kwenye matokeo positive ya mwisho
Over confidence inaweza kukufanya upoteze mchezo huku upande wa pili ile Jihad ya kuona wao ni dhaifu hivyo wakajituma kwa nguvu zote wanaweza kupata ushindi dhidi ya timu bora.
Hata tulivtofungwa hapa na Jwaneng Galaxy msimu uliopita, haikuchangiwa na ubovu wa kikosi ilikuwa ni over cinfidence.
Wakati wapinzani walikuja kucheza Jihad na kwa bahati mbaya au nzuri wenzetu wakashinda.
Hizi References zenu za Derby ni ishara jinsi gani wengi wenu hamshirikishi ubongo, juzi hapo Man U kamfunga Arsenal licha ya kwamba Arsenal ni bora zaidi ya Man kwa msimu huu lakini ubora wake haukumsaidia japo kuwa mpira walicheza sana na kufanya mashambulizi mengi.