FT: Simba 2-0 Yanga | NBC PL | Benjamin Mkapa Stadium | 16.04.2023

FT: Simba 2-0 Yanga | NBC PL | Benjamin Mkapa Stadium | 16.04.2023

Mwanamuziki nguli wa Bongofleva, Lady Jay Dee aliwahi kuimba kibao maarufu " Siku hazigandi " alikuwa sahihi. Lile pambano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu hatimae ndio linapigwa leo, ama kweli siku hazigandi.

Ndio ni Kariakoo Derby, ni Simba Sc Vs Yanga Sc katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam saa 11:00 jioni.

Mnyama mkubwa mwituni, Simba Sc itakuwa inawaalika wapinzani wao wa jadi Yanga, huku ikijaribu kupunguza pengo la point baina ya timu hizo mbili.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na alama 68 huku Simba ikiwa na alama 60 hivyo kufanya tofauti kuwa alama 8 huku zikisalia mechi 5 kabla ya msimu kuisha.

Simba itashuka dimbani kujaribu kutafuta ushindi wake wa kwanza tangu ilivyofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2019. Ni mechi saba sasa Simba hajamfunga Yanga katika Ligi Kuu ya NBC.

Mechi ya mwisho walipokutana wababe hao, matokeo yalikuwa 1-1 kwa magoli ya Augustine Okrah kwa Simba na Aziz Ki kwa upande wa Yanga.

Simba itashuka dimbani huku ikimtegemea zaidi mshambuliaji wake aliyefomu , Jean Baleke ambaye kwasasa hakamatiki kwa fomu yake huku akina Chama, Ntibazonkiza na Mzamiru wakitegemewa kuleta chachu ya ushindi.

Kwa upande wa Yanga, watamtegemea zaidi Straika wao ambaye fomu yake imekuwa ikipanda na kushuka Fiston Kalala Mayele huku pia Aziz Ki na akina Jesus Moloko wakitegemewa kunogesha zaidi.

Je, Simba atakubali kuendelea kuwa mnyonge kwa Yanga?
Na vipi upande wa pili, ubingwa bila kumfunga mtani unaweza kunoga?

Mwamuzi wa mtanange huo ni mwanamama, Jonesia Rukya akisaidiwa na akina Janeth Balama pamoja na Mohamed Mkono.

Mechi ni saa 11:00 jioni na itakuwa live Azam Sports 1HD

Kwa live updates, utani wa hapa na pale na yote yanayohusu mechi hii basi hapa ndio sehemu sahihi kwako Mwana JF...

View attachment 2589925
Kikosi cha Simba
View attachment 2589930
Kikosi cha Yanga
Timu zinaingia uwanjani
Mchezo umeanza
2' Goooooooooooooooooooo
Inonga anafunga goli kwa kichwa baada ya walinzi wa Yanga kuzubaa
5' Mchezo una kasi, Yanga wanajipanga kutafuta goli la kusawazisha
10' Mvua imeanza kunyesha uwanjani
18’ Mchezo umesimama kwa muda Inonga ameumia baada ya kugongana na Musonda
22' Mchezo unaendelea, ufundi umepungua kiasi kutokana na mvua
29’ Shuti la Baleke linagonga nguzo baada ya kupewa pasi nzuri na Chama
29’ Kibu Denis anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
31’ Yanga wanapata kona ya 3
32’ GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Kibu Denis anafunga goli la pili kwa shuti kali
43' Baleke anakosa nafasi nyingine ya wazi akipokea pasi ya Chama
45' Zinaongezwa dakika 2

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza
45' Mabadiliko kwa Yanga, ametoka Sure Boy ameingia Azizi Ki
Ametoka Yaniki Bangala ameingia Mudathiri Yahya
Ametoka Moloko ameingia Tuisila Kisinda
47' Mayele yupo chini ameumia
56’ Djuma Shaban anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Saido
65’ Mchezo umesimama kwa muda ili kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji kufturu
67’ Mchezo unaendelea
69’ Azizi Ki almanusura afunge, shuti linatoka nje kidogo ya lango
70’ Mabadiliko kwa Yanga, anatoka Musonda anaingia Bernard Morrison
74' Mabadiliko kwa Simba, anatoka Erasto Nyoni anaingia Kapama
82' Simba wanamtoa Baleke anaingia John Bocco
90' Zinaongezwa dakika 5

Full Time
Tangu 2019 ,Simba HAIJAWAHI kumfunga yanga
Screenshot_20230417-070810.jpg
 
Refarees wa bongo zero kabisa,hilo goli la kwanza limetokana na makosa ya refaree na wasaidizi wake
 
Picha linanza,baada ya mechi nikatupia uzi wangu,the nikatoka kuelekea dukani kupata japo soda,ile nakunja kona namuona mtoto mmoja mkaleeeeeeeeeeeeee,katupia uzi wa mnyama kashika vuvuzela,akanicheki kisha akatabasamu nikampa hi,akareply nikamwambia nakaa paleeeeeee,in case utataka tuangalie marudio.

Mtoto akasema si nakuonaga uko na demu ako,mnaenda kununua ice cream,nsije kupigwa buree mie,nikamwambia yule utopolo,hii wiki ni ya wanyama hebu weka namba hapa mtoto.

Mnieombee wazinzi wenzangu furaha ya simba inanipa gono sio mdaa mimi dah[emoji25][emoji25][emoji25]
Wanarudia lini na saa ngapi mkuu
 
Nilichokuwa nakitaka ndio hiki kimetokea leo.

Ishu haikuwa sio tu kumfunga Yanga

Bali ni kumfunga Yanga akiwa full compact plus na vile virutubisho vyake vya jezi nyeusi kuihusisha na bahati.

Mwaka jana niliposikia taarifa kuwa Mayele anataka kuuzwa mpaka Senzo kutishia kuondoka endapo atauzwa, nilikuwa mtu niliye tofautiana mtizamo na baadhi ya mashabiki wenzangu wa Simba.

Mimi sikutaka hilo litokee, hiyo yote ilikuwa kwa ajili ya siku kama ya leo.

Tungewafunga wakiwa wamepungukiwa na wale wachezaji wao nyota ningefurahi kama ushindi kumfunga mtani ila vibe lingekuwa too low.

Kwasababu kile kipindi tuwafunge bao 4-1 ni ukweli usiopingika kuwa hawakuwa na kikosi bora. That's why unaona hata wao utetezi wao ulikuwa "tulikuwa tuna kikosi kibovu"

Leo kila waliyetaka kumuona uwanjani, alikuwepo.

Kuanzia benchi la ufundi mpaka wachezaji wote leo walikuwepo, hakukuwa na majeruhi, hakukuwa na wachezaji waliokosa mechi sababu ya kadi za njano.

Leo labda watafute lawama kwa kumkosa Feisali. (Kitu ambacho nitawaona vigeugeu kwasababu wao ndio waliosema no Feisali no problem)

Mwisho nasema mjifunze kuiheshimu Simba, muache ushamba wa kuamini rangi ya jezi kuwa ndio yenye bahati.

Mechi yenu inayofata aanzeni upya hesabu zenu, kuanzia ule ukiritimba wa kufurahia kila mechi kufunga goli hadi unbeaten
Simba tayari mna kombe lenu la msimu.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom