FT || Simba Sc 2 Vs 2 CSKA Moscow

FT || Simba Sc 2 Vs 2 CSKA Moscow

Wachezaji Simba wanatosha hakuna haja tena ya kusajili striker. Akikukosa Bocco una maliziwa na Kyombo, huku Kibu D mwalimu anampika anakuja kuwa moto vibaya mno. Kwa mpira huu dhidi ya CSKA Moscow, Yanga wapambane washinde mechi zao zote maana Simba haitapoteza mechi. Halafu klabu bingwa kosa kosa nusu fainali.
 
Nimeona kipindi cha kwanza chote live baina ya CSKA VS Simba, kama Simba beki Mohamed Quattara ameendelea vile vile kuonyesha uzembe anapocheza nafasi ya ulinzi, kibaya zaid kapangwa na Onyango, wote hawana akili, nguvu nyingi maarifa kidogo.

Kocha Robertinho ananitia wasiwasi, kiungo Erasto Nyoni hajacheza takriban mechi 15 pale Simba, amekuwa akisugua benchi sana na wakati mwingine tulibashiri anapelekwa kwa mkopo, Leo kaanza kiungo wa chini kwa timu ambayo ukubwa wake kila mtu anaujua.

Nina wasiwasi sana huyu kocha time will tell

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app

Mkuu kwani kazi ya kocha ni nini?kwa hyo mnataka hao kina nyoni wawekwe mechi za maana au sio!!??hapa anawajaribu awaone uwezo wao,ndo maana ya mechi za kirafiki kila mtu anacheza..acheni ushamba wa kudhani kila mechi mnataka kushinda tuuu mbona iko wazi hizi ni mechi za majaribio tu.
 
Bahati yao watoto wa Moscow
Nasikia ilibidi tuachie hapo hapo kwenye 2-2, putin alitishia tukifunga vijana wao la 3 anapiga bomu uwanjani na pale makao makuu msimbazi [emoji23]
Mkuu eti inasemekana wa Putin walitaka kuhakikisha vita za silaha za moto kuja kwenye mpira wa mguu. Walitaka kuhakikisha watu wanapigwa wiki, ila muwekezaji (Mo) akawapoza hasira na kuwaambia wawe waungwana wataamsha vita vilivyolala kwa wana msimbazi na kwa bahati mbaya leo ndio dirisha linafungwa. Nongwa zitakuwa nyingi hivyo tusaidiane kufunika kombe.
 
Yaani watu wana sherekea mechi ya kirafiki kutoa sare. Hakika kweli faraja ni jambo la muhimu katika maisha ya binadamu ukikosa basi fosi hata upumbavu ukupe furaha.
Kuna watu tangu wazaliwe hawajawahi kushuhudia timu yao inacheza na timu ya Ulaya
 
Nimeona kipindi cha kwanza chote live baina ya CSKA VS Simba, kama Simba beki Mohamed Quattara ameendelea vile vile kuonyesha uzembe anapocheza nafasi ya ulinzi, kibaya zaid kapangwa na Onyango, wote hawana akili, nguvu nyingi maarifa kidogo.

Kocha Robertinho ananitia wasiwasi, kiungo Erasto Nyoni hajacheza takriban mechi 15 pale Simba, amekuwa akisugua benchi sana na wakati mwingine tulibashiri anapelekwa kwa mkopo, Leo kaanza kiungo wa chini kwa timu ambayo ukubwa wake kila mtu anaujua.

Nina wasiwasi sana huyu kocha time will tell

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
Ulitaka ucheze wewe ?
 
Yaani watu wana sherekea mechi ya kirafiki kutoa sare. Hakika kweli faraja ni jambo la muhimu katika maisha ya binadamu ukikosa basi fosi hata upumbavu ukupe furaha.

Sa ulitaka walie[emoji2957]
 
Mbivu na mbichi itajulikana kwenye michezo ya kimashindano. Kama unakumbuka msimu ambao mnatolewa kwenye klabu bingwa na Galaxy, Simba ilicheza michezo ya kirafiki ya kimataifa na vilabu vya maana tu na haikupoteza mechi. Lakini ilipokuja mechi za kimashindano ikaleta taswira tofauti. Mechi ya kirafiki mnayosherekea nayo au kubezwa nayo kwa matokeo haiwezi ku reflect chochote katika mechi za kimashindano
ndio maana Nabi wetu huwa anajichagulia Friends Rangers, wala hana hata hamu na timu za Afrika Kaskazini au Ulaya
 
Walishangilia kwenye mechi ya kirafiki? Walishangilia kwenye mechi inayokuongeza point. Sasa sare mliyopata inaongeza point kwenye mashindano yapi?
Ingekuwa mechi ya kirafiki haina impact yoyote, basi wala wewe usingekuwapo hapa unamwaga povu
 
Back
Top Bottom