FT: Simba SC 3-1 Singida Big Stars | Estadio Benjamin Mkapa | 03/02/2023

Majira ya Saa 1:00 Usiku kwa Masaa ya Afrika ya Mashariki,Mnyama mkubwa mwituni, Simba SC watashuka dimbani katika dimba la Benjamin Mkapa kuwakaribisha wana alizeti Singida Big Stars.

Mechi inategemewa kuwa ngumu, maana katika mchezo wa kwanza pale Liti, Singida, timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 1-1.

Simba itashuka dimbani ikiwategemea wachezaji wake mahiri kama Chama, Saido, na wengineo huku Singida Big Stars ikiwategemea zaidi akina Bruno, Kazadi na mastaa wengneo.

Je, Simba ataweza kuzoa alama zote tatu? Au Singida ndio atakayeibuka kidedea? Tukutane saa 1:00 usiku kwa live updates...

Ubashiri wangu: Simba 2-1 Singida
2_1
 
Kikosi cha Simba SC Kinachoanza dhidi ya Singida Big Stars
FB_IMG_1675436519138~2.jpg
 
Tujiandae kisaikolojia Makolo wenzangu,kipigo leo hakikwepeki, tulikuwa tunashadadia mkataba wa Yanga tukasahau game yetu
Mtu akishadadia mkataba kuna shida Gani kwani Wanasimba ndo walisaini huo mkataba. Muwe mnaajiri watu wenye upeo wa kutosha.
 
Majira ya Saa 1:00 Usiku kwa Masaa ya Afrika ya Mashariki,Mnyama mkubwa mwituni, Simba SC watashuka dimbani katika dimba la Benjamin Mkapa kuwakaribisha wana alizeti Singida Big Stars.

Mechi inategemewa kuwa ngumu, maana katika mchezo wa kwanza pale Liti, Singida, timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 1-1.

Simba itashuka dimbani ikiwategemea wachezaji wake mahiri kama Chama, Saido, na wengineo huku Singida Big Stars ikiwategemea zaidi akina Bruno, Kazadi na mastaa wengneo.

Je, Simba ataweza kuzoa alama zote tatu? Au Singida ndio atakayeibuka kidedea? Tukutane saa 1:00 usiku kwa live updates...

Ubashiri wangu: Simba 2-1 Singida
Kipigo atakachoambulia kolo leo kitazika ndoto yake ya kuwa bingwa wa nbc premier league mwaka huu. Mbaya zaidi, hapo kesho, 4/2/2023 robertinho anatupiwa virago.
 
Kwasababu striker wako Kibu hajaanza?
Nimeuliza kwasababu watu walimponda Chama, kuwa mzungu anapenda mpira wa kasi na Chama hafai kwenye mfumo wa mzungu. Sasa ndio najiuliza hiki kikosi kaachiwa Mgunda apange au mzungu kaishapata mfumo wa Chama?
 
Back
Top Bottom