FT: Simba SC 7-0 Horoya AC | CAF Champions League | Benjamin Mkapa | 18.03.2023

FT: Simba SC 7-0 Horoya AC | CAF Champions League | Benjamin Mkapa | 18.03.2023

Bila kusahau ka kibwagizo
p_6832124121384522232757_0_5e7075bc9850341bc4dd7edf10dd5eca.jpg
 
Mnyama Mkubwa Mwituni asiyefugika, Simba Sports Club anashuka dimbani leo kuikabili Horoya AC katika mchezo muhimu wa kundi C.

Simba itaingia uwanjani ikiwa na alama 6 huku Horoya wakiwa na alama 4. Ushindi wa aina yoyote utawafanya Simba wafuzu robo fainali.

Leo ni ama afe kipa au afe beki, ushindi ni lazima kwa Mnyama, na kwa uzoefu wangu, mechi za namna hii Simba akiwa kwa Lupaso huwa tunashinda goli zisizopungua 3.

Shime wana Simba tujitokeze kwa wingi hapo Lupaso ili tukahanikize ushindi wetu mapema, najua friends of Horoya watakuwepo ila hawatosumbua.

Mchezo utakuwa mubashara saa 1:00 usiku na kama kawaida, ZBC 2 ya AzamTv na Variety 4 ya DStv watakuwa live.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Simba Sports Club. [emoji881][emoji881][emoji881]
Bila kusahau star times nao hawako nyuma kwa hili, wanaonyesha mechi zote za michuano hii bila kuchagua mechi
 
Wanawachukulia poa horoya halafu ushindi wa vipers umewasahaulisha kwamba wao ni wabovu , sasa leo ndo ile siku watu wanaenda kuaibika
Unavyohangaika kama kuku anayetaka kutsga!! Umeona wapi simba wakiichukulia poa horoya?.
 
Hongera Simba kwa kufuzu nusu fainali sisi zetu dua uende zaidi ya hapo Nenda Simba Nenda [emoji123]
 
Hii mechi ngumu sana ,naona ni kama fainal ,Simba wakaze sana aisee ikiwezekana wafie uwanjan Leo .
Tunachotaka ni ushindi tu Hakuna kingine.
Mungu wabarik wachezaj wetu wakawe na utimamu wa akili na juhudi.
 
Back
Top Bottom