FT: Simba SC 7-0 Horoya AC | CAF Champions League | Benjamin Mkapa | 18.03.2023

FT: Simba SC 7-0 Horoya AC | CAF Champions League | Benjamin Mkapa | 18.03.2023

Unstoppable[emoji173]
9609956fcfc740302321bb9ceb445eaa.jpg
 
Kama hatujafilisi bajeti yote ya serikali sijui. Huu ni uhujumu uchumi 🤣😂🤣
Ni kweli, ila hatuna haja ya kufikiria hizo hela maana tukiingia tu robo fainali tuna zaidi ya 1.4B. Hizo tuwaachie Yanga wapige nazo picha
 
Mnyama Mkubwa Mwituni asiyefugika, Simba Sports Club anashuka dimbani leo kuikabili Horoya AC katika mchezo muhimu wa kundi C.

Simba itaingia uwanjani ikiwa na alama 6 huku Horoya wakiwa na alama 4. Ushindi wa aina yoyote utawafanya Simba wafuzu robo fainali.

Leo ni ama afe kipa au afe beki, ushindi ni lazima kwa Mnyama, na kwa uzoefu wangu, mechi za namna hii Simba akiwa kwa Lupaso huwa tunashinda goli zisizopungua 3.

Shime wana Simba tujitokeze kwa wingi hapo Lupaso ili tukahanikize ushindi wetu mapema, najua friends of Horoya watakuwepo ila hawatosumbua.

Mchezo utakuwa mubashara saa 1:00 usiku na kama kawaida, ZBC 2 ya AzamTv na Variety 4 ya DStv watakuwa live.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Simba Sports Club. 🦁🦁🦁

====
Kikosi cha Simba SC

Timu zinaingia uwanjani
Mchezo unaanza
2' Timu zinasomana mchezo
5' Simba wanaongeza kasi ya mashambulizi
10' Goooooooooo
Chama anafunga goli kwa faulo ya moja kwa moja
15' Simba wanakosa nafasi ya wazi baada ya Kibu Denis kuteleza
20' Horoya wanaonesha kujibu mashambulizi
27' Kidogo kasi ya mchezo imepungua lakini timu zote zinatengeneza mashambulizi
29' Kadi ya njano kwa Kibu Denis
31' Gooooooooo
Baleke anafunga goli la pili
35' Penatiiii kwa Simba baada ya mlinzi wa Horoya kuunawa mpira
Gooooooo
Chama anaipatia Simba goli la tatu kwa penati
45' Zinaongezwa dakika 2

MAPUMZIKO: Simba wanaongeza kwa Magoli 3-0

Hongera Mtani

Finali hii hapa...Shida ni Mamelodi na Al Ahly. Mkitoboa hapo huyu hapa Raja Casablanca kwenye fainali
 
Back
Top Bottom